PWANI:HOSPITALI YA WILAYA YA MKURANGA HAINA X-RAY
Wakazi wa wilaya ya Mkuranga mkoani Pwani wameilalamikia hospitali ya wilaya hiyo kwa
kutokuwa na huduma ya x-ray na hivyo
kuwalazimu wakazi hao kwenda kupata
huduma hiyo katika hospitali za taifa Muhimbili jijini Dar es salaam.
Wakazi hao wamesema kuwa kukosekana kwa huduma ya
X-ray katika hospitali hiyo kuna wasababishia gharama za kwenda muhimbili jijini Da es
salaam kwa ajili ya kupata huduma.
Mwenyekiti wa chama cha maendeleo chadema wilayani humo Rwey Jamal amesema kuwa
hospitali hiyo haikutakiwa kuitwa hospitali badala yake ingeitwa kituo cha afya
kwani kutokuwepo kwa huduma hiyo ni tatizo kubwa hasa kwa hospitali ya wilaya.
Mganga mkuu wa hospitali hiyo Dr Francis Manisi amethibitisha
kutokuwepo kwa mashine hiyo na kudai
kuwa wako mbioni kuweka huduma hiyo kwani imekuwa changamoto kubwa kwa wagonjwa
hali ambayo huwafanya walipe kiasi kikubwa cha fedha kwenda katika hospitali ya
taifa
Post a Comment