RORYA:WAUMINI WA DINI MBALIMBALI WATAKIWA KUWA NA USHIRIKIANO
Waumini
wa dini mbalimbali wametakiwa kuwa na ushirikiano katika shughuli za kiroho ili
kukuza mahusiano mazuri na kujenga umoja bila kubaguana kwa sababu za
kiitikadi.
Kauili
hiyo ilitolewa na mwenye kiti wa kijiji cha Deti Sebastiani Okaro wakati wa
harambee ya kuchangia vyombo vya muziki vya kanisa la Waadventista Wasbato la
Radienya lililoko kata ya Labuor Wiyani Rorya.
Okaro
ameyasema hayo baada ya kuona kuwa hakuna waumini wa dhehebu liingine
walioalikwa kutoa michango yao hali ambayo iliwafanya waumini hao kushindwa
kufikia malengo waliyojiwekea.
Amesema
kuwa endapo madhehebu yatakuwa na umojo wa kiundungu wataongeza imani kwa wale
ambao hawajaamua kumfuata Mungu na kwanjia hiyo tabia na mienendo yao
itabadilika na kupunguza uharibifu katika Wilaya hiyo.
Naye
mgeni rasmi wa harambee hiyo Cuthbert Simion aliwataka waumini kutumia mali zao
katika ujenzi wa makanisa kama ilivyo wanavyotoa kwenye harusi na misiba.
Katika
harambee hiyo zaidi ya sh.2.1 milion zilikusanywa kwa ajili ya ununuzi wa
vyombo vya muziki vitakavyo wafanya waimbaji wa kwaya ya kanisa hilo kumtukuza
Mungu ndani na nje ya Wilaya ya Rorya huku lengo likiwa ni kupata sh, 3.5
milioni.
Post a Comment