MTANGAZAJI

KIGOMA:SERIKALI YAPIGA MARUFUKU WAJAWAZITO KWENDA KUJIFUNGULIA KWA WAGANGA



Serikali Wilayani Kibondo katika Mkoa wa Kigoma imepiga marufuku vitendo vya akina mama wajawazito kwenda kujifungulia kwa waganga wa kienyejibadala yake kwenda hospitalini.

Mkuu wa Wilaya hiyo Venas Mwamoto amesema kuwa bado wakina mama wengi wajawazito wanakwenda kujifungulia kwa waganga wa kienyeji hali inayosababisha kuongezeka kwa idadi ya vifo.

Mkuu huyo wa wilaya amesema kuwa waganga wakienyeji watakao bainika kuwalaghai wajawazito watachukuliwa hatua za kisheria kwani kazi hiyo inapaswa kufanywa na wataalamu wa liopo katika hospitali na vituo vya afya.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Dr Emanuel  Mwasulama amebainisha kuwa katika kila wanawake wajawazito 100 ishirini na tano kati yao wanajifungulia kwa waganga wakienyeji.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.