ARUSHA:WAKAZI WA TEMI YA SIMBA WAOMBA MSAADA
Wakazi wa kijiji cha Temi ya simba kata ya bwawani akipokea misaada |
Wananchi wa kitongoji cha
Nyamagana,kijiji cha Temi ya Simba,kata ya Bwawani katika Jimbo la Arumeru
Magharibi mkoani Arusha wameziomba Taasisi mbalimbali za kiserikali na Dini
kuongeza misaada zaidi ya chakula,malazi,na mavazi kutokana na maafa ya
mafuriko yaliyowapata kati ya mwezi wa April na Mei mwaka huu.
Akizungumza na Vyombo
vya Habari hivi karibuni kwa niaba ya wananchi mwenyekiti wa kijiji cha
Temi ya Simba Emanuel wiliam Molel amesema kuwa wanakijiji hao
wanakabiliwa na njaa,Malazi,mavazi pamoja na Nyumba baada ya mafuriko kutokea
mnamo machi 23 Mwaka 2014 na kuathiri shughuli za kiuchumi katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa Taarifa
kutoka kwa mwenyekiti huyo Nyumba Arobaini na Tisa zilianguka hivyo
kuwafanya wakazi wa kijiji hicho kukosa makazi.
Kanisa la waadventista
wasabato Kijenge limekabidhi kwa wananchi hao misaada yenye thamani ya
shilingi milioni moja za kitanzania,misaada hiyo ni mahindi,maharage,na
Nguo.Hata hivyo serikali ya kijiji iliweza kuwapatia pia Magodoro,Nguo na
chakula.
Post a Comment