DODOMA:RAIS KIKWETE KUTANA NA MAWAZIRI HII LEO
Rais Jakaya Kikwete leo anatarajia kufanya kikao cha Baraza la Mawaziri mjini Dodoma kabla ya kuwasilishwa kwa Bajeti Kuu, bungeni kesho.
Kikao hicho cha Baraza la Mawaziri kinakaa huku kukiwa na vuta ni kuvute katika Kamati ya Bajeti ya Bunge ya kupitisha vifungu mbalimbali vinavyoonekana kuleta utata kwenye bajeti hiyo .
Wakati Wabunge wakihoji sababu ya serikali kuendelea kutegemea wafadhili katika bajeti yake badala ya kukusanya mapato ya ndani, wamehoji pia matumizi yasiyoyalazima kuendelea kuwekwa kwenye bajeti hiyo.
Taarifa zinaeleza kuwa Rais alitarajiwa kuwasili leo Dodoma na kikao hicho kinafanyika hii leo .
Kamati ya Bajeti inayoongozwa na Mwenyekiti, Andrew Chenge, ilianza kujadili bajeti hiyo tangu Jumatatu.
Spika wa Bunge, Anne Makinda, juzi aliahirisha Bunge ili kuipisha Kamati hiyo iweze kukaa kwa siku mbili kujadili mambo muhimu kama ilivyo kawaida ya Bunge la Bajeti.
Wajumbe wengine waliomo kwenye kamati hiyo ni Christine Lissu, Kidawa Hamid Saleh, Mansoor Shariff, Amina Abdallah Amour, Joseph Selasin, Dk. Cyril Chami, Dk. Bulugu Limbu, Assumpter Mshama, James Mbatia, Beatrice Shellukindo na Hamad Rashid Mohamed.
Chanzo:Nipashe
Post a Comment