MTANGAZAJI

WAKRISTO NA WAISLAMU NCHINI UGANDA WAMSHUKURU RAIS WAO KUPINGA USHOGA

Raia wa Uganda kutoka dini mbali mbali, jana wamekusanyika katika uwanja wa Kololo mjini Kampala kwa maombi maalum na kutoa shukurani kwa Rais Yoweri Museveni kwa kutia saini mswaada wa sheria unaozuia mapenzi ya jinsia moja.

Hii ni mara ya kwanza viongozi wa dini za kikristo na waislamu nchini Uganda kujitokeza kwa pamoja na kuandaa Ibada maalum ya kumshukuru Rais Museveni na kuliombea taifa kuepuka vitendo vya ushoga.


Ibada hiyo maalum imefanyika baada ya karibu mwezi mmoja na nusu tangu Rais Yoweri Museveni kuiidhinisha sheria hiyo ambayo raia wengi wa nchi hiyo wameipigia debe huku kukiwa na shinikizo kubwa kutoka kwa mataifa ya Magharibi yakimtaka Rais Museveni kubadili msimo wake, na baadhi ya mataifa yakipunguza msaada kwa Ugand
a
.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.