WAKALA WA MAABARA YA MKEMIA MKUU WA SERIKALI YAANDAA SEMINA YA MATUMIZI SALAMA YA KEMIKALI KWA WAANDISHI WA HABARI NA TAASISI MBALIMBALI
Ofisi ya
Mkemia Mkuu wa Serikali na Msajili wa Kemikali za Viwandani na Majumbani
ameandaa mafunzo juu ya Matumizi Salama ya Kemikali kwa ajili ya
waandishi wa vyombo vya habari (TV,Radio na Magazeti) na asasi zisizo za
kiserikali zinazojihusisha na utoaji wa elimu kwa umma kuhusu matumizi
salama ya Kemikali.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo hayo wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa ufunguzi wa mafunzo. Mafunzo
hayo yanafanyikia kwenye ukumbi wa Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa
Serikali uliopo ndani ya jengo la "Mkemia House" barabara ya BarackObama
(Zamani Ocean Road)
Washiriki wa mafunzo wakifuatilia Mafunzo
Kaimu Mkemia Mkuu wa Serikali Ndugu Samanitho Mtega (Katikati) akifungua mafunzo juu ya Matumizi Salama ya Kemikali. Kushoto kwake ni Bi. Everlight Matinga-Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na Udhibiti wa Kemikali. Kulia kwa Kaimu Mkemia Mkuu wa serikali ni Kaimu Meneja wa Kanda ya Mashariki ndugu Daniel.
Mkurugenzi wa
Idara ya Sayansi ya Makosa ya Jinai (Forensic Science) na Vinasaba Bi. Gloria Cuthbert Omary ametoa wito kwa waandishi wa Habari kuwa kiungo kati ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali na Jamii
katika kuelimisha na kuleta upatanisho kati ya taasisi hiyo na Jamii
ili jamii iweze kujifunza na kuelewa juu ya kazi mbalimbali zinazofanywa
na Wakala hiyo.
Bi. Gloria amesema kuwa waandishi wa habari wana wajibu wa pekee katika kujenga taifa kwa kuandika habari
zilizo sahihi kutoka mamlaka husika na kuongeza kuwa kwa kufanya hivyo
watatoa mwanya kwa wanajamii na wadau mbalimbali kuchangia kwa usahihi
hoja na mijadala inayohusiana na kazi au matokeo ya Uchuguzi unaofanywa
na Wakala wa Mabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali nchini Tanzania.
WADAU WA KEMIKALI WAZINGATIE SHERIA NA KANUNI
Wadau wa Kemikali nchini wametakiwa
kufuata Sheria na Kanuni wakati wa kuingiza, kusafirisha, kuhifadhi,
kuuza, kusambaza na wakati wa kutumia kemikali hizo ili kuepusha madhara
yanayoweza kuletwa na matumizi yasiyo salama ya kemikali.
Hayo yamesemwa na Bi. Everlight Matinga
ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Usimamizi na Udhibiti wa
Kemikali (katika ofisi ya Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali)
wakati akitoa ufafanuzi kwenye mafunzo hayo kuhusu sheria ya Kemikali za
Viwandani na Majumbani ambayo lengo lake ni kulinda afya za wananchi na
mazingira
Post a Comment