SHERIA MPYA YA ADHABU KWA WANAOVAA NUSU UCHI YAPITISHWA NCHINI UGANDA
Rais wa Uganda, Yoweri Museveni,
ametia saini sheria mpya inayotoa adhabu kali kwa wanaopatikana na hatia ya
kutembea nusu uchi au kuhusika na vitendo vinavyohusisha picha zenye watu uchi.
Wanawake pia wamezuiwa kabisa
kuvalia sketi fupi sana au 'Mini Skirt' kama zinavyojulikana au blausi ambazo
zinaonyesha kifua chao hadharani na kusababisha hisia za kingono .
Sheria hiyo inasema kuwa nguo kama
hizo zitakubalika tu ikiwa zinatumika kwa ajili ya mafunzo au wakati wa michezo
na hafla za kitamaduni.
Akihutubia waandishi wa habari,
mjini Kapmala, waziri wa maadili na utawala bora, Reverend Simon Lokodo alisema
kuwa Rais Museveni alipitisha sheria hiyo tarehe 6 mwezi huu, miezi mwili bada
ya bunge kuipitisha.
Kwa mujibu wa sheria hiyo kamati
dhidi ya vitendo hivyo itabuniwa ili iweze kutekeleza sheria hiyo kwa
kuhakikisha kuwa picha, au video zenye watu uchi zinanaswa na kuharibiwa.
Kamati hiyo, itajumuisha watu kutoka
katika sekta mbali mbali ikiwemo ya habari na utumbuizaji.
Sheria hiyo inasema kuwa mtu yeyote
atakayepatikana akijihusisha na vitendo cya watu kuwa uchi, kuvalia nusu uchi ,
kuona sinema za watu wakiwa uchi au kuchapisha picha za watu walio uchi kwa
lengo la kuleta hisia tofauti utachukuliwa hatua kali za kisheria.
Waziri alisema kuwa serikali haitaki
watu kuvalia nguo zisizo na heshima na kuzua hisia zisizofaa miongoni mwa watu.
Watakaopatikana wakivunja sheria na
kuvalia visivyo watafungwa hadi miaka 10 na wale watakaopatikana na hatia ya
kuhusisha watoto katika biashara ya ngono watafungwa hadi miaka 15.
Chanzo:BBC
Post a Comment