MTANGAZAJI

UTAFITI UNAONESHA KUWA TATIZO LA UBAKAJI BADO NI KUBWA TANZANIA

Tatizo la Ubakaji nchini Tanzania bado ni kubwa,Ripoti ya Utafiti wa Ukatili wa Kijinsia ya Chama cha Wamahabari Wanawake Tanzania (TAMWA) iliyotolewa leo Aprili 19,2014 inaonesha kuwa Wanafunzi wa shule za msingi na sekondari wanabakwa,wanapewa mimba na kukatisha masomo,huku wanawake vikongwe wakibakwa katika maeneo mbalimbali ya Tanzania kutokana na imani za kishirikina au ulevi wa kupindukia.

Ripoti hiyo inatokana na utafiti uliofanyika Tanzania Bara katika wilaya za Kahama,Tarime,Sengerema,Newala,Mbulu,Singida Vijijini,Bariadi,Busega,Nkasi,Dodoma,Babati,Chunya na Bunda,Kwa upande wa Zanzibar ni katika wilaya za Mjini Magharibu,Kusini Pemba,Kaskazini Pemba,Unguja Kusini na Kaskazini Unguja.

Katika Ripoti hiyo takwimu zinaonesha kuwa katika kipindi cha mwaka 2011/12 kesi za ubakaji zilizoripotiwa kwa jeshi la Polisi Tanzania zilikuwa ni 93,zilizofikishwa mahakamani ni 7,zilizotolewa hukumu ni 4 na ambazo zilizofutwa ni 3.

Mwaka 2012/13 kulikuwa na kesi za ubakaji zilizoripotiwa kwa jeshi la Polisi Tanzania  79,zilizofikishwa mahakamani ni 11 na zilizotolewa hukumu ni hakuna.

Utafiti unaonesha kuwa kesi zote 242 za kubaka zilizoripotiwa kwa mkoa wa Kaskazini,kesi chache ndizo zinazofikishwa mahakamani kutokana na vikwazo tofauti,rushwa ikitajwa kuwa ni miongoni mwa vikwazo hivyo,ambapo ilibainika kuwa kituo cha Polisi Mahonda mwaka 2012 kilipokea kesi 30 za kubakwa kati ya hizo ni kesi 8 tu zilizopelekwa mahakamani na kesi moja tu ilipata Uamuzi,Aidha kesi 30 zilizofikishwa mahakama ya mfenesini na kesi 7 tu ndizo zilipatikana na hatia.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.