CHANGIZO LA HOSPITALI YA PASIANSI MWANZA YA WAADVENTISTA WA SABATO KUFANYIKA MACHI MOSI,2014
Picha ya Jengo la Hospitali ya Pasiansi hapa ilikuwa Aprili,2013 |
IDARA ya Afya na Kiasi ya Kanisa la Waadventista wa Sabato, katika Jimbo la Nyanza Kusini inatarajia kufanya changizo maalum kwa ajli ya kumalizia ujenzi wa Hospitali ya Rufaa inayojengwa pasiansi jijini Mwanza.
Mkurugenzi wa Afya na Kiasi wa Jimbo hilo,Dk. Silasi Kabhele, amesema changizo hilo litafanyika Machi Mosi mwaka huu,litatanguliwa na juma rasmi la maombi na kufunga, na kisha kutolewa sadaka maalum kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo.
Kwa mujibu wa Dk.Kabhele, hospitali hiyo ya Mwanza Adventist Medical Centre ambayo jiwe la msingi liliwekwa Septemba mwaka jana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dk.Jakaya Mrisho Kikwete, ujenzi huo unatarajiwa kukamilika mapema mwaka huu.
Hospitali hiyo inatarajia kuwa na jumla ya vitanda 450 vya kulaza wagonjwa mbalimbali;ikiwa ni pamoja na chuo cha sayansi ya tiba na uuguzi.
Hospitali hiyo inayojengwa kwa nguvu za wananchi na michango mbalimbali inatarajia kugharimu jumla ya shilingi za Tanzania Bilioni 62.4.
Aidha, Dk.Kabhele amesema, hospitali hiyo itakapoanza kazi itakuwa ikihudumia wagonjwa 250 kila siku ,ikitibu magonjwa mbalimbali yakiwemo magonjwa ya moyo,kisukari na saratani ambayo yamekuwa yakiigharimu serikali mamilioni ya fedha za kigeni kusafirisha wagonjwa kwenda nje ya nchi kufanyiwa uchunguzi na tiba.
Mkoa wa Mwanza, sasa una Hospitali moja ya Rufaa ya Bugando, Hospitali hiyo ya Pasiansi itakapokamilika, itakuwa Hospitali kubwa ya tatu ya Rufaa Mkoani Mwanza. Hospitali nyingine ni Sekou Toure,ambayo iko mbioni kupandishwa hadhi kutoka kuwa Hopitali ya Mkoa wa Mwanza ili kuwa ya Rufaa.
Hata hivyo Kufuatia hali hiyo,Mkurugenzi huyo wa Afya na Kiasi wa Jimbo la Nyanza Kusini, ametoa mwito kwa washiriki wa Kanisa la Waadventista wa Sabato na wananchi wengine wa ndani na nje ya Nchi kuichangia hospitali hiyo siku hiyo ya Machi Mosi Mwaka huu.
Post a Comment