Tamasha la Imba kwa Upendo lilifanyika PTA jijini Dar es salaam Februari 23,2014 ambalo lilihusisha vikundi vya nyimbo za Injili vya Kanisa la Waadventista Wa Sabato vya jijini humo.
Tamasha hilo ambalo lilidhaminiwa na JCB Studioz zilizopo Tegeta kwa ushirikiano na blog ya mtangazaji liliwakutanisha waimbaji binafsi na vikundi zaidi ya 10 lilikuwa ni kwa ajili ya kuvikutanisha na kujenga mahusiano kwa vikundi hivyo na studio za JCB katika kufanikisha uimbaji katika masuala ya uinjilisti, kurekodi,matangazo na masoko.
Picha zote kwa hisani ya JCB Studioz |
Post a Comment