MTANGAZAJI

AJINYONGA BAADA YA RAFIKI YAKE KUFARIKI DUNIA

Mkazi mmoja wa kijiji cha kewanja kata ya matongo wilayani Tarime mkoani Mara Mwita Nyasinge (30)amejinyonga hadi kufa baada ya rafiki yake kipenzi kufariki dunia kwa kudaiwa kupigwa na walinzi wa mgodi wa north Mara baada ya kukutwa akijaribu kuingia katika eneo la mgodi huo mapema februari 19,mwaka huu. 

Kwa mujibu wa chanzo chetu Marehemu alifariki usiku wa februari 23 kwa kujinyonga kwa kamba chanzo kikiwa ni hasira na uchungu wa rafiki yake kipenzi kupoteza maisha Hata hivyo kwa mujibu wa habari toka wilayani humo zinasema kuwa marehemu hakuona haja ya kuendelea kuishi baada kuona rafiki yake kipenzi amefariki dunia hali ambayo ingepelekea yeye kuishi maisha yasiyo na Amani na hivyo kuamua kuchukua uamuzi wa kujinyonga .

 Chanzo hicho kimeeleza kuwa marehemu Chacha Mgima Marwa alikamatwa na walinzi wa mgodi huo wa North Mara Februari 19 majira ya usiku akitafuta mchanga wa dhahabu ambapo baada ya saa chache kesho yake februari 20 alipelekwa katika Kituo cha afya cha Sungusungu Nyamongo akiwa hajitambui. 

Hali ya afya yake ilidhoofika na kukimbizwa katika hospitali ya KKKT Shirati ambapo alifariki dunia februari 22 na mwili wake umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti hospitali ya wilaya ya Tarime. 

Kutokana na hali hiyo familia imekataa kuuchukuwa mwili wa marehemu kwa maziko ikidai kuwa wanahitaji kufahamu ndugu yao alivyofariki kwa kuwa alimkamatwa akiwa hai.

 Hata hivyo juhudi za mwandishi wa habari hii kutoka Mara kumpata msemaji wa jeshi la polisi hazikufanikiwa haraka kulisemea hili. .

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.