UZINDUZI WA TOLEO LA PILI LA DVD LA NJIRO SDA CHOIR-ARUSHA HUU HAPA
Kwaya ya Kanisa la Waadventista
Wasabato Njiro jijini Arusha inataraji kuzindua toleo lake jipya la video
linaloitwa “TUMAINI LENYE BARAKA”lenye nyimbo nane.
Uzinduzi huo ambao Mgeni Rasmi
atakuwa ni Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato nchini Tanzania Mch Dr
Godwin Lekundayo utafanyika katika viwanja vya Kanisa la Waadventista Wasabato
Njiro Juni 30,2013 kuanzia saa 7 mchana ambapo pia kutakuwa na Kwaya ya Kijenge
na Sakina zote za jijini humo.
Post a Comment