TAKWIMU ZA HUDUMA ZA KIJAMII NCHINI TANZANIA
Utafiti wa
Viashiria vya VVU,UKIMWI na Malaria Tanzania kwa mwaka 2011 hadi 2012 uliofanywa
na Ofisi ya Taifa ya Takwimu kwa kushirikiana na Ofisi ya Mtakwimu Mkuu wa
Serikali ya Zanzibar unaonesha kuwa,Kaya nchini Tanzania zinawastani wa watu
watano,karibu robo ya kaya zinaongozwa na wanawake,Karibu nusu ya wananchi wana
umri chini ya miaka 15.
Hali ya
maisha imekuwa bora kwa kiasi Fulani katika maeneo ya mijini Tanzania bara na
Zanzibar kuliko maeneo ya vijijini Tanzania Bara.
Karibu kaya
tisa kila kaya kumi za mijini Tanzania Bara zinapata maji ya kunywa kutoka
katika chanzo kilichoboreshwa,ukilinganisha na
asilimia 47 ya kaya za vijijini Tanzania Bara.
Karibu kila
mahali Zanzibar kuna vyanzo vya maji ya kunywa vilivyoboreshwa.Huduma za usafi
wa mazingira zipo kiwango kidogo nchi nzima asilimia 26 kwa kaya za mjini Bara
na asilimia 7 tu ya kaya za vijijini Bara ndizo zenye huduma bora za usafi wa
mazingira.
Kaya sita
katika kila kaya kumi Zanzibar zinapata huduma bora ya usafi wa mazingira.
Asilimia 15
ya kaya Tanzania ndizo zenye umeme,idadi imeongezeka kidogo kutoka asilimia 12
ya mwaka 2007 na 2008.Tanzania Bara kuna tofauti kubwa katika upatikanaji wa
umeme baina ya kaya za mijini na vijijini
ambapo ni asilimia 46 tu. Kwa upande wa Zanzibar asilimia 41 ya kaya ndio
zenye umeme.
Zaidi ya
asilimia 60 ya kaya nchini Tanzania zina redio,wakati asilimia 15 tu ndizo
zenye tv,Asilimia sitini na moja ya kaya zina simu ya mkononi.Karibu kaya moja
katika kila kaya tano zina akaunti
benki.Karibu nusu ya kaya zina baiskeli wakati asilimia 2 tu ya kaya
zina gari dogo au lori.
Asilimia
kumi na nane ya wanawake wenye umri wa miaka 15-49 na asilimia 9 ya wanaume
wenye umri huo hawana elimu.Zaidi ya nusu ya wanawake na wanaume wamehitimu
elimu ya msingi.Ambapo asilimia moja tu ya wanawake na asilimia 2 ya wanaume
wamehitimu elimu ya sekondari ama zaidi.
Wanaume
wanauwezekano mkubwa wa kupata habari kupitia vyombo vya habari kuliko wanawake
nchini Tanzania.Zaidi ya asilimia 40 ya wanawake hawakuwa na uwezo wa kupata
taarifa kupitia vyombo vya habari angalau kwa kila juma ukilinganisha na
asilimia 23 tu ya wanaume.
Redio ni
njia inayotumiwa na wengi kupata taarifa kwani asilimia 74 ya wanaume na
asilimia 49 ya wanawake wanasikiliza redio kila juma.
Post a Comment