VIJANA WA TANZANIA NA VVU
Utafiti wa viashiria vya VVU/UKIMWI na Malaria Tanzania mwaka 2011 hadi 2012 uliotolewa mwaka 2013 na Tume ya kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) unaonesha kuwa asilimia tisa ya wasichana na 10% ya wavulana wenye miaka 15-20 waliripotiwa kujamiana kwa mara ya kwanza kabla ya kutimiza miaka 15.
Miongoni mwa wenye miaka 18-24,alisilimia 50 ya wasichana na 43% wa wavulana waliripoti kufanya ngono wakiwa na miaka 18.
Ngono kabla ya Ndoa:
Utafiti huo unaonesha kuwa karibu theluthi moja ya wasichana ambao hawajawahi kuolewa na 42% ya wavulana ambao hawajawahi kuoa walikuwa wamejamiana miezi 12 kabla ya utafiti.Wasichana ambao hawajawahi kuolewa wana uwezekano mkubwa wa kuripoti kwamba hawajawahi kujamiana 59% kuliko wavulana ambao hawajawahi kuoa asilimia 48.
Miongoni mwa vijana wenye miaka 15-24,karibu nusu ya wasichana na theluthi- moja ya wavulana wamewahi kupima VVU na kupokea majibu yao.
Wasichana na wavulana wenye miaka 20-24 wanauwezekano mkubwa wa kuwa wamewahi kupima VVU na kupokea majibu kuliko wasichana na wavulana wadogo zaidi miaka 15-19
Post a Comment