WAZIRI MKUU WA TANZANIA KUUNDA TUME KUCHUNGUZA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda ameunda Tume maalum itakayofanya uchunguzi wa matokeo ya mtihani wa kidato cha nne ambayo yalitangazwa na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Dk. Shukuru Kawambwa Februari 18, mwaka huu.
Katika matokeo hayo yaliyotangazwa februari 18 mwaka huu , asilimia 60 ya
wanafunzi waliofanya mtihani wa kidato cha nne Oktoba, 2012 walifeli.
Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Peniel Lyimo amesema Tume hiyo
ambayo inatarajiwa kuanza kazi wakati wowote wiki ijayo inajumuisha
wadau kutoka Chama cha Wamiliki wa Shule na Vyuo Binafsi (Tanzania
Association of Managers and Owners of Non-Government Schools/Colleges
(TAMONGSCO), Taasisi za Dini zinazotoa huduma ya elimu, Chuo Kikuu cha
Dar es Salaam na Asasi zisizo za Kiserikali (NGOs) zinazoshughulikia
masuala ya elimu.
Wadau wengine watatoka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Kamati ya
Bunge ya Huduma za Jamii na Umoja wa Wakuu wa Shule za Sekondari
Tanzania (TAHOSSA).
Amesema Serikali inawaomba wadau wa elimu, wazazi, walezi na wananchi
wote kwa ujumla watoe ushirikiano kwa Tume ili iweze kufanya kazi yake
kwa ufanisi.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 3021,
DAR ES SALAAM.
JUMAMOSI, FEBRUARI 23, 2013.
Post a Comment