MTANGAZAJI

TAARIFA YA SAVE THE CHILDREN KWA VYOMBO VYA HABARI


Kutumiwa vibaya kwa jina la Save the Children kuiba pesa kutoka kwa familia maskini

Hivi karibuni, Save the Children ilipata taarifa kuwa kuna kikundi cha watu wanaodai kuwa ni wafanyakazi wa Save the Children wanaozunguka katika vijiji mbalimbali vya wilaya za Moshi na Same wakisajili watoto yatima na waishio katika mazingira magumu. Watu hao walikuwa wakikusanya kile walichodai ada ya usajili kwa ajili ya msaada wa masomo, kiwango cha kuanzia Sh. 50,000 hadi 70,000. Tulitoa taarifa polisi kuhusiana na kitendo hicho na mara moja polisi mkoani Kilimanjaro iliwakamata watu watatu kuhusiana na suala hilo.

Save the Children imesikitishwa sana na kitendo hicho cha kuiba pesa kutoka kwa watu maskini ambao walikuwa wakiamini kuwa wanatoa kwa ajili ya shirika linalosaidia watu wenye shida katika jamii. Kitendo hicho si tu kwamba ni kosa la jinai, bali ni cha aibu na si cha kiungwana.

Tuengependa kuweka wazi kuwa watu hao hawakuwa na uhusiano wowote na shirika letu, bali walikuwa ni matapeli.

Save the Children inafanya kazi ya kuboresha maisha ya watoto ulimwenguni kote. Kila shilingi tunayoipata nchini Tanzania na kwingineko, inatumika kusaidia watoto wenye mahitaji katika jamii na tunalaani vitendo vyovyote vinavyokwenda kinyume na malengo hayo. Hatutozi ada yoyote kwa huduma tunazozitoa katika jamii.
 
Rachel Pounds,

Mkurugenzi wa Save the Children nchini Tanzania


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.