MTANGAZAJI

WAKUU WA MIKOA WAPYA NCHINI TANZANIA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, amewateua wafuatao kuwa Wakuu wa Mikoa.

Dkt. Rajab Mtumwa RUTENGWE ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa KATAVI. Kabla ya hapo Dkt. Rutengwe alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Mpanda.


Ndugu Magalula Saidi MAGALULA ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa GEITA. Kabla ya hapo Ndugu MAGALULA alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi.


Ndugu Paschal Kulwa MABITI ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa SIMIYU. Kabla ya hapo Ndugu MABITI alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida.


Kapt. Asery MSANGI ameteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa NJOMBE. Kabla ya hapo Kapt. MSANGI alikuwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa.

Uteuzi huu unaanza tarehe 
15 Machi, 2012. Wataapishwa Ikulu, Dar es Salaam, Jumatano tarehe 21 Machi, 2012 saa 04:00 asubuhi.


Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
15 Machi, 2012

1 comment

Mustapha MaDish said...

Kinachotakiwa ni kazi bora!!
So wachape kazi hasa!!

Mtazamo News . Powered by Blogger.