MTANGAZAJI

ZIARA YA KIONGOZI WA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO DUNIANI TED WILSON KATIKA NCHI ZA AFRIKA MASHARIKI

Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wasabato Duniani Ted Wilson akizungumza na waandishi wa habari nchini Burundi,kushoto kwake ni Kiongozi wa Kanisa hilo kanda ya Afrika Mashariki na Kati  Blasious Ruguri, na Nancy ambaye ni mke wa Ted Wilson.

Ted Wilson akizungumza na waumini nje ya Kanisa la Waadventista Wasabato la Jabe March 6, 2012. palipo na kituo cha radio na hotuba ya kiongozi huyo ilirushwa  na Kituo cha Televisheni cha Taifa cha Burundi.

Jumla ya watu wapatao 40,000 walikusanyika kwenye uwanja wa Amahoro mjini Kigali,Rwanda ambapo Ted Wilson alihudutubia umati huo na hii ilikuwa ni robo ya watu waliokuwepo uwanjani hapo Machi 3, 2012

Mama Nancy Wilson akitambulishwa kwa watu waliokuwa kwenye uwanja wa  Amahoro akiwa amevalia vazi la asili la wanawake wa Kinyarwanda. Kutokana na umati mkubwa uliojitokeza siku hiyo robo tatu ya wananchi wa Rwanda walisikiliza kilichokuwa kikifanyika uwanjani hapo kupitia kituo cha radio cha FM .

Machi 6,2012 Ted Wilson alikutana na Rais wa Burundi  Pierre Nkurunziza ofisini kwa rais huyo kwa mazungumzo maalum.(Picha zote kwa hisani ya  Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kanisa la Waadventista Wasabato Afrika Mashariki na Kati Steven Bina)

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.