MTANGAZAJI

MWANAHABARI ABSALOM KIBANDA AACHIWA HURU BAADA YA KUHOJIWA NA POLISI

Absalom Kibanda ambaye ni Mhariri Mtendaji wa Free Media Ltd na Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri ameachiwa huru baada ya kuhojiwa kwa saa 3 Makao Makuu ya Jeshi la Polisi, Dar es Salaam kwa uchochezi.

Ameachiwa kwa damana ya ahadi ya Sh5 milioni aliyowekewa na Mhariri wa Mwanahalisi, Saed Kubenea na anatakiwa kuripoti tena Makao Makuu ya Polisi Jumatatu saa 3. asubuhi.


Kuhojiwa kwa Kibanda kunafuatia makala ya Samson Mwigamba ambaye ni mchangiaji katika gazeti la Tanzania Daima aliyoitoa Jumatano, Novemba 30, 2011 akiwahamasisha polisi wa chini kukataa amri za wakubwa wao zenye mlengo
 wa kutekeleza maslahi ya kisiasa.
Mwigamba tayari amefunguliwa mashtaka kwa  kosa la uchochezi.

Neville C. Meena,

 Katibu  Jukwaa la Wahariri nchini Tanznia,  Dar es Salaam -Tanzania.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.