Marehemu Priscus Makiluli ndani ya Ukumbi
Ni ajali iliyotokea Disemba 11,2011) baada ya arusi ya Edith Malima na Isaack Nkya.Huduma ya kufunga harusi ilianza mnamo saa 5 asubuhi, katika kanisa la Chuo Kikuu cha Arusha ikiongozwa na Pr Nzungu.
Baada ya hapo ilifuatiwa na sherehe ya harusi katika ukumbi wa Rash Garden jijini Arusha. Baada ya sherehe kwisha mnamo saa 3 usiku msafara wa magari kuelekea majumbani (U0A) ulianza.
Msafara huu ulijumuisha magari ya kukodi ( Hice) na magari binafsi. Gari aina ya Hice ijulikanayo kwa jina la Jiga ilipofika maeneo ya kwa mrefu iligongana na costa na kupelekea Hice kutumbukia mtaroni ikiwa imeharibika vibaya.
Ajali hiyo ilisababisha vifo vya watu wawili Priscus Makiluli na Annah Johnson Mseli ambaye ni mke wa Mch Mseli Mbaya Majeruhi katika ajali hiyo ni 1 Mr Buriro – Project Accountant UoA ambaye ameumia mguu na mkono Mrs Buriro- ambaye amepata jeraha katika macho yote mawili Mrs Mbega – secretary wa DFA – ameumia mkono Mr Chamliho- mkufunzi kitengo cha Elimu- amepata jeraha na kushonwa katika paji la uso 5Mrs Mwashinga- jeraha dogo Mr Mabula Tobe – Mwanafunzi Mwaka wa kwanza kitengo cha theologia- ameumia mkono 7 Hawa John – Mwanafunzi kitengo cha Elimu maumivu mwilini. 8Mrs Majula – Mke wa mzee majula ambaye ni Patron TASS ameumia mkono 9 Janeth Mwakalila – Mwanafunzi kitengo cha biashara – Jeraha Mguuni 10. Mrs Kaduma – Mguzi katika zahanati yetu ya Chuo – amepata maumivu kifuani. 11. Glad Arego- Mototo wa Mwl Simon Arego. Maumivu mwilini. 12. Mrs Mkongo – Jeraha kubwa mguuni 13. Pr Mseli Mbaya – amevunjika mkono na mguu ambaye yeye hakuonekana baada ya ajali ila mnamo leo saa tatu asubuhi alipatikana katika hospitali ya Seliani. 14. Mrs Nziku – amepata jeraha mguuni. 15. Dereva wa gari aina ya Hiace ambaye amevunjika miguu . Baada ya ajali kutokea washuhudiaji waliofika awali katika eneo la tukio wakiwemo wale waliotoka kwenye harusi, walisaidiana na wananchi wengine wa eneo la kwamrefu naku wahisha majeruhi pamoja na maiti katika hospitali ya Mountmeru .
Marehemu Priscus Makiluli -Alizaliwa mwaka 79 -Alikuwa ni mkimya -Mchapakazi :Hili limezungumzwa na wafanyakazi wanafunzi na jumuia nzima ya chuokikuu cha Arusha. -Aliwahi kuwa Accountant pia Treasure katika shule ya Bupandagila. -PA Payment Accountant Chuokikuu cha Arusha -Ameacha mjane na mtoto mmoja mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi miwili
Marehemu Mama Mseli Mbaya Ameacha mme na watoto wawili wote wakiwa wakiume, wa kwanza Reuben Mseli miaka 15 anaingia kidato cha tatu TASS anaitwa Jonsoni Mseli anayetarajia kuingia darasa la saba 2012 TAPS. Na William Izungo
|
Post a Comment