MTANGAZAJI

CHUO KIKUU CHA ST.JOHN CHAFUNGWA

Vurugu za wanafunzi wa Chuo Kikuu cha St. John mkoani Dodoma za
kuushikiza uongozi uwape fedha za kujikimu zimeibuka tena jana na
kusababisha chuo hicho kufungwa hadi Januari 3, mwakani.

Hali hiyo imeibuka jana asubuhi ambapo wanafunzi wa shahada ya kwanza

wa mwaka wa kwanza hadi wane, walipoendelea kuushinikiza uongozi wa
chuo hicho kuwapa fedha za kujikimu.

Mgomo huo ulianza Jumatatu wiki hii, ambapo wanafunzi hadi

walikusanyika na kuutaka uongozi kuwapa fedha za kujikimu kwa madai
wao hawana fedha.

Aidha, mgomo huo ulishindwa kuendelea baada ya Kikosi cha Kutuliza

Ghasia (FFU) kufika chuoni hapo na wanafunzi hao kutimua mbio.

Hali hiyo iliendelea kuwa tete baada ya wanafunzi hao jana asubuhi

kurudi tena na kuanza mgomo upya huku wakiendelea kuushinikiza uongozi
huo kutoa fedha hizo.

Wanafunzi hao walikuwa wametanda kwenye eneo la Utawala la chuo hicho

huku wakipiga kelele na wengine wakirusha mawe.

Kutokana na vurugu hizo, chuo kiliamua kuomba msaada polisi ambapo

magari matatu ya FFU yalitanda chuoni hapo kwa ajili ya kuwatawanya
wanafunzi hao.

Uamuzi wa kufungwa kwa chuo hicho ulitolewa na uongozi wa chuo huku

polisi wakiwa wametanda na mabomu ya machozi.


  Chanzo: http://www.ippmedia.com/frontend/index.php?l=36661

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.