MTANGAZAJI

MAKUBALIANO YA MHESHIWA KIKWETE NA CHADEMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete na ujumbe wa serikali yake pamoja na viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), wakiongozwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Mheshimiwa Freeman Mbowe leo, Jumatatu Novemba 28, 2011 wamemaliza mkutano wao wa siku mbili Jijini Dar es salaam kuhusu Muswada wa sheria ya mabadiliko ya Katiba wa Mwaka 2011.

Mkutano huo uliofanyika Ikulu umefanyika katika mazingira ya maelewano


Pande mbili zimekubaliana kama ifuatavyo:-


1.Pamoja na sheria hiyo kupitishwa na Bunge ipo haja ya
  kuendelea kuiboresha ili ikidhi mahitaji na kujenga kuaminiana na muafaka wa Kitafa.

2.Kwamba yawepo mawasiliano na mashauriani ya mara kwa mara

kati ya serikali na wadau mbalimbali juu ya kuboresha sheria hiyo kwa lengo
la kudumisha muafaka wa Kitaifa kwenye Katiba Mpya.

Imesainiwa na;


Mhe.  John Mnyika-Kaimu Katibu wa Chadema

Mhe. John Emmanuel Nchimbi-Waziri wa Habari,Vijana na Michezo

2 comments

Anonymous said...

juzi bunge lilipokea taarifa ya kamati ya jairo. moja ya hadidu za rejea ilikuwa kama mchakato ulikiuka HAKI ya bunge.
kwenye suala hili la muswada wa katiba wabunge wa chadema na nccr mageuzi waliondoka bungeni na matokeo yake muswada ukapishwa. sasa wameamua kukutana na rais na kuzungumza naye kwa kuwasilisha maoni yao ambayo kimsingi hayatengui kupishwa muswada huo.

kitendo hiki ni kuudhalilisha muhimili wa nchi ambao ni bunge. walitakiwa kuchangia kwa upana bungeni na wananchi wangeona hoja zao na kuziunga mkono lakini kukimbia uwanja wa kutolea hoja nadhani si haki kwa wananchi tuliowapigia kura

Anonymous said...

rekebisheni neno mheshimiwa lisomeke vema badala ya mheshiwa

Mtazamo News . Powered by Blogger.