MTANGAZAJI

UNAYO HABARI KWAMBA ARDHI YAKO IMEIBWA??

Mashirika ya fedha (Hedge Funds) ni miongoni mwa taasis zinazoongoza kuiba/kupora ardhi ya  Afrika ili kujiongezea faida katia miradi yake, hasa katika sekta za chakula na nishati (biofuel). Haya yamesemwa na taasis moja ya kitafiti ya Marekani.
 
Katika ripoti yao, taasis hiyo ya Oakland Institute imesema mashirika hayo ya fedha pamoja na wawekezaji wengine wa kimataifa wamekuwa wakipora ardhi ya Waafrika kwa kutumia mikataba mibovu.

Ripoti hiyo inaendelea kusema kwamba mashirika na wawekezaji hao wamekuwa wakijitwalia ardhi hiyo kiubabaishaji na kupelekea wakulima wadogo wa Kiafrika kunyang'anywa ardhi yao ya asili.
Mpango huu ni mahsusi kabisa katika mpango wa kuhodhi biashara ya chakula na nishati itokanayo na mazao ya chakula.

Oakland Institute imeendelea kusema kwamba mashirika na wawekezaji hawa wanapotwaa ardi hizo badala ya kuzalisha chakula, wamekuwa wakifanya kilimo cha nishati na maua.

"Hili ni tishio kubwa kwa binadamu kuliko hata ugaidi. Wizi na Unnyang'anyi huu unatishia uwepo wa chakula cha kutosha kwa binadamu." Inasema sehemu ya ripoti hiyo.

Taasis hiyo imesema imetoa ripoti hiyo baada ya kufanya utafiti wa kina katika nchi za Ethiopia, Tanzania, Sudan ya Kusini, Sierra Leone, Mali, na Msumbiji.
Kuna Mwafrika atakayepona kwenye hili kweli?
Maelezo zaidi soma hapa ama hapa

1 comment

Anonymous said...

Hii ni kweli kabisa,
ukifika Arusha waweza kurithibitisha hilo. Mashamba makubwa ya Maua,Maeneo makubwa yanamilikiwa na Wazungu kwa kigezo cha uwekezaji au makazi, hayapo tena mikononi mwa watanzania wazalendo. Ni mali ya walowezi wa Kizungu.
Muze

Mtazamo News . Powered by Blogger.