MTANGAZAJI

ASSA KUZINDUA ALBAMU YAO YA AUDIO NAMBARI SITA KESHO

Kutoka kulia ni Mkuu wa Maburudisho wa Chama cha Vijana wa Kiadventista wanaosoma katika Shule za Sekondari zilizopo Dar es salaam,Zanzibar na Pwani na Mwenyekiti wa Kwaya ya ASSA Kabula Mpenzwa  akiwa na Mhazini Msaidizi wa Chama hicho Monica Mang'ombe wakiwa katika Studio za Morning Star Radio leo baada ya mahojiano katika kipindi cha Lulu za Injili kuhusu uzinduzi wa Albamu ya ASSA toleo nambari 6 itakayozinduliwa kesho jumapili  katika Shule ya Sekondari ya Azania jijini Dar es salaam saa 7:00  mchana hadi saa 12:00 jioni.Miongoni mwa waimbaji watakaokuwepo ni Acacia Singers,The Voice,The Heroes na wengine wengi.Kiingilio ni bure

1 comment

salasala said...

Ninafurahi sana kuona kazi ya Mungu inaendelezwa na vijana wa ASSA. Njozi yakurekodi ilianza mwaka 2002 na ndipo tukafanikiwa kutoa kanda ya kwanza chini ya uongozi wa mwenyekiti Noah Mathew. Ninafurahi kuona hii njozi inaendelezwa na neno la Mungu linasambaa kote kote. Nafurahi ninaposikia nyimbo za wanassa. Mungu awabariki sana

Mtazamo News . Powered by Blogger.