MTANGAZAJI

MGOMO WA DALADALA TENA MJINI MOROGORO

Mkazi wa mjini Morogoro akitembea kwa miguu na wanae baada ya mgomo wa magari ya daladala mijini humo. 
(picha na Juma Mtanda)

Tokea jana hapa Morogoro kumetokea Mgomo wa Madereva wa Daladala, wakipinga kutozwa Ushuru wa kutokea Stand ya Daladala hizo kwani huwa wanatozwa Tsh 300/= kila trip mojo. Mbunge wa Morogoro Mjini Mheshimiwa Aziz Abood amejitolea kutoa Mabasi yake ya Abood Bus Service kusafirisha wanafunzi Mashuleni.

Mgomo huo utachukua Takriban siku tatu tokea jana, wao Madereva wanataka watozwe Tsh 500/- kwa kutwa lakini siyo kwa kila trip. Hiyo sehemu  inayoshughulika na ukusanyaji wa Mapato hayo ni ya Kigogo mmoja.
Na DUSTAN OSCAR

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.