JE WAJUA VUVUZELA LINA MADHARA???
VUVUZELA chombo kilichotumika kwa kushangilia hasa na mashabiki wa  soka kwenye Kombe la Dunia la soka mwaka 2010, si tu kinachafua  mazingira kwa kelele, wataalamu wanadai chombo hicho kinaweza  kusababisha maradhi kiafya mpulizaji.
 Inaeleza kwamba upulizaji kidogo tu wa Vuvuzela mfanya mpulizaji  atokwe na mate mengi sawa na yanayotoka wakati mtu akipiga chafya, tena  yenye uwezo wa kusafiri hewani kwa mwendo kasi mara milioni nne kwa  sekunde moja kwa kila tone, hii ni kwa mujibu wa jarida moja la  kimataifa
Inaelezwa kuwa eneo lililofurika watu, mtu mmoja akipuliza vuvuzela  linaweza kuwaathiri watu wengi kwa magonjwa yanayosambazwa kwa kuvuta  hewa kama mafua na kifua kikuu.
Hata hivyo, Dk. Ruth McNerney, aliyeendesha utafiti wa hivi karibuni  katika shule inayohusika na masuala ya usafi na maradhi ya nchi za joto  ya London – London School of Hygiene & Tropical Medicine, anasema  “upulizaji wa chombo cha vuvuzela” huenda kinahitajika kuliko kukipiga  marufuku.
“Kama ilivyo wakati wa kukohoa na kupiga chafya, hatua zinapaswa  kuchukuliwa kuzuia uenezaji wa maradhi, na watu wenye maradhi ya  kuambukiza washauriwe wasipulize vuvuzela zao karibu na watu”, alisema.
Kamati yake iliyochunguza hatari zinazoletwa na upulizaji wa  vuvuzela, waliowatumia watu wanane waliojitolea kupuliza vuvuzela. Kwa  wastani chembechembe zinazotoka kwenye mapafu, 658,000 kwa lita ya hewa  zilitolewa kutoka kwenye vuvuzela.
Matone hayo ya mate yaliruka angani kwa kiwango cha mara milioni nne  kwa sekunde. Kwa kulinganisha, wakati watu hao waliojitolea walipotakiwa  kupiga kelele, waliweza kutoa mate kiasi cha chembechembe 3,700 tu kwa  lita kwa kiwango cha 7,000 kwa sekunde.


Post a Comment