MTANGAZAJI

MABOMU YA MACHOZI DODOMA

WANAFUNZI Chuo Kikuu cha Dodoma jana waliweza kutimuliwa  na mabomu na askari wa Kikosi cha Kuzia Ghasia (FFU) baada ya kushinikiza waruhusiwe kuingia kushiriki mjadala wa Muswada wa mabadiliko wa Sheria wa Katiba katika viwanja vya Bunge.

Askari hao walilazimika kuwatimua wanafunzi hao baada ya kutokea vurugu kutokana na anafunzi hao kufunga barabara iendayo mkoani Morogoro ili waweze kushiriki muswada huo jamboambalo halikuafikiwa.

Wanafunzi hao walitaka kushfiriki musawada huo baada ya kuona wamedharauliwa na Bunge hilo kwa kualikwa shule za Sekondari na kluachwa wao wanachuo.

Wakiongea eneo la tukio wanafunzi hao walisema kuwa hawakubaliani na matakwa ya bunge ya kutengeneza katiba pasipo kuwashirikisha wananchi wenyewe na endapo wakipitisha katiba hiyo wataingilia kati ikiwemo na kuandamana ili kupinga maamuzi hayo kwa kuwa katiba hiyo ni manufaa kwa watu wote.

“Inaonekana huko bungeni kuna kikundi cha watu wachache wanaotughilibu na wanataka kujitengenezea katiba ya kujilinda na kujinufaisha wao na mambo yao kwa manufaa yao, na wameona wakitushirikisha sisi wasomi tutagundua na kukataa” walilalama.

Hata hivyo, Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt. James Msekela alishindwa kuzuia ghasia hizo kwa kuzomewa na wanafunzi hao na hatima yake aliruhusu askari hao kuwafanyia mashambulizi wanafunzi hao kwa kukaidi.


Hata hivyo mkuu huyo alidai ukumbi uliotengwa kutumika kujadili rasimu huo ni mdogo na wanafunzi hao walikubali kutuliza ghasia baada ya mbunge Lema kuwataka kutuliza ghasia hizo kwa kuwa yeye ndie aliataka wanafunzi hao washiriki kwa kuwa muswada huo umeandikwa kwa lugha ya Kiingereza.

Wanafunzi hao walipiga kelel kutaka kubadilishwa wka ukumbi na hatima yake walitawanya kwa mabomu ya machozi kuondoka mahali hapo.



No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.