MTANGAZAJI

RAIS KIKWETE AANGUKA JUKWAANI JANGWANI

Walinda usalama wakiwa wamembeba Mgombea wa Urais kupitia Chama cha Mapinduzi CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa amebebwa na usalama wa Taifa baada ya kuanguka ghafla wakati alipokuwa akihutubia umati wa wanachama cha CCM waliohudhuria katika Uzinduzi wa kampeni za chama hicho kwa ajiri ya kampeni za uchaguzi wa Urais, Wabunge , Madiwani utakaofanyika mwezi Oktoba 31 mwaka huu.

Akina mama wakilia kwa uchungu baada ya Mgombea wao wa urais kupitia chama cha mapinduzi CCM. Rais Jakaya Kikwete baada ya Kuanguka ghafla wakati akihutububia wafuasi wa chama hicho jangwani.

Kikwete akiwapungia mkono wana ccm baada ya kurejea tena katika jukwaa baada ya kupewa matibvabu hata hivyo amelazimika kufungua swaumu yake.

Pwani Raha.com imeeleza kuwa sehemu ya viwanja vya Jangwani inaweza kuwa na historia mbaya kwa Jakaya Kikwete kwani mwaka 2005 alianguka katika mazingira kama hayo wakati akitoa hutuba ya kufunga kwa kampeni upande wa chama chake cha CCM.
(Picha na http://www.pwaniraha.com/)


1 comment

Mashughuli said...

huna habari nzito kaka

Mtazamo News . Powered by Blogger.