MTANGAZAJI

TUSEME UKWELI KUHUSU UKIMWI

Jamani janga la ukimwi ni kubwa sana katika jamii ya kiafrika na tunahitaji kupigana vita kubwa kabisa kuukabili ukimwi, lakini wengi wetu tumejikita katika aina moja ya vita dhidi ya ukimwi aina hii ya vita ni ile ua ushawishi wa watu juu ya matunizi ya kondomu kama njia lahisi kabisa ya kujikinga na ukimwi na hii ndo imekuwa silaha pekee ya kila mtu anayezungumzia jambo lolote kuhusu ukimwi.

Serikali na pia wanaharakati woote kwa pamoja wanasisitiza sana juu ya matumizi ya kondomu kila kona ya nchi hii na hata wengine kupendekeza elimu ya matumizi ya kondomu ipelekwe mpaka mashuleni watoto wetu wapate kuielewa vizuri.

Sisi sote ni kama tumekuwa katika mtizamo mmoja wa vita hii na aina ya silaha tunayo tumia kupigana na ukimwi silaha zingine zoote zimeonekana kuwa kama hazifai katika mapambano dhidi ya ukimwi,tangu ukimwi uibuke hapa kwetu ni zaidi ya miaka inakaribia miaka 30 tangu 1984 hadi leo maambukizi yamekuwa yakiongezeka kila kukicha.

Tumehimiza watu kupima kwa hiari na watu wamejitokeza kupima, njia nyingine zoote tumezihubili lakini imeshindikana janga la ukimwi bado linaendelea kuitafuna nchi lakini tatizo hapa hatulioni katika hii vita na kama tunaliona hakuna anayedhubuti kulisemea kwa vile ni kama watu woote tumekuwa kama watumwa wa ukimwi kwa hiyo tumechagua silaha moja tu nayo ni matumizi ya kondomu.

Lakini mimi nasema na nawaambia ndugu zangu watanzania woote popote pale tulipo kuna mambo tunayaona lakini tunashindwa kuyasema kama ndio chimbuko hasa la ukimwi moja ya mambo haya kubwa kabisa ni mmomonyoko wa maadili, watanzania ni kama tumepagawa kwa ngono hata tukifanyaje hata tukivaa kondomu kumi kwa wakati mmoja kama hatukubadili tabia na mienendo ya maisha yetu ukimwi utatumaliza, ngono inatisha jamani tubadili tabia hii ndo njia pekee ya kubadili mfumo mzima wa vita dhidi ya ukimwi.

Kuna mambo ambayo yanachangia ukimwi kuenea kwa kasi kufuatia hicho nilichokisema kama ni mmmonyoko wa maadili katika jamii yetu na ili tuweze kuhimili vita hii ya ukimwi kwa kuzingatia kuwa ni kuporomoka kwa maadili katika jamii lazima tupigane vita ifuatayo kama kweli tunahitaji kuliepusha taifa na janga la ukimwi,

1. kufuta leseni zoote za nyumba zoote zinazoendesha biashara ya kulala wageni maarufu kama guest house kwa sababu nyumba hizi ndo chanzo hasa cha maabukizi ya ukimwi, kila kona ya miji ya tanzania kila mtaa kuna guest house ukiuliza wanalala kina nani ni aibu.

2. zile nyumba zoote zitakazoruhusiwa kuwa za kulala wageni zikiwemo hotel itungwe sheria ambayo itatamka bayana wale watakaoruhusiwa kulala humo kama ni mwanaume na mwanamke wawe na cheti cha ndoa.

3 bar zenye guest house bubu zipigwe marufuku.

4.jamii na kila familia ihamasike na kulichukulia suala la maadili kama changamoto inayotukabili hasa kuanzia ngazi ya familia, kila familia idhibiti mienendo isiyoeleweka ya wana familia.

mfano watoto wa kike na wa kiume kutoka na kudhurura ovyo muda waoote badala ya kufanya shughuli za kujiingizia kipato, eneo hili likidhibitiwa vema itawasaidia pamoja na wale vijana waliopotea katika janga la kubwia unga, hili ni moja wapo ya familia kutokuwa makini na wafamilia na hatimaye watoto kujiingiza katika mambo yasiofaa.

Hayo ndo yanayo tusumbua lakini hatupendi kuyasema kwa vile watu woote tumekuwa watumwa wa ngono nani asiyejua kinachofanyika katika guest house na hasa dar,watoto wa shule humo, wake za watu humo, waume za watu humo, vyuo humo, watoto wa mitaani humo kila uchafu wa ngono unafanyika humo mpaka aibu, kwa nini tunashindwa kupigana vita katika hili badala yake tunakimbilia matumizi ya kondomu then tunasema tuko katika vita dhidi ya ukimwi?

Mimi nasema hatuko katika vita dhidi ya ukimwi bali tunatangaza biashara ya kondomu!! Yako maeneo ukifika unashangaa kabisa mpaka unajiuliza hivi serikali ipo? viongozi wapo? wale wapiganaji wa ukimwi tupo? je hatuoni mambo haya? wapo watu wasamabaza ukimwi makusudi huku wakijua ni makosa vipi hawa watu na basi ikiwezekana tusifichane tusemane waziwazi ukigundulika una ukimwi watu tuambiwe jamani furani anao ili kujiepusha ma majanga ya kuingiliwa na watu wasio na huruma na wengine! kwa nini tunaogopa kutangazana hadharani?

Tutunge sheria kudhibiti mambo haya na ziwe kali ili kulilinda taifa, sheria iseme wazi baba mtu mzima unaongozana na mtoto wa shule sio mtoto wako unampeleka wapi?unaingia nae guest na wahudumu wanakupa chumba kwa nini? kwa nini usichukuliwe hatua kwa kitendo kama hicho?

Yako pia maeneo yanalalamikiwa kuwa ni chanzo cha maabukizo ya ukimwi maeneo haya ni salon! eneo hili nalo liangaliwe salon za kike zichunguzwe kama lengo lake ndilo au kuna mambo mengine yanafanyika humo! hakuna vita yoyote utakayopigana ukichekeana na adui yako! vita havina macho, kama tumeamua kupambana na ukimwi tuamue kweli si huu utani tunaofanya kuhimiza watu kutumia kondom na kuwafundisha jinsi ya kuzivaa hii tunacheza hatutafanikiwa kamwe! bila sheria kali hakuna kitu!

TUSEME UKWELI TUSIWE WANAFIKI SABABU ZA MAABUKIZI YA UKIMWI KUZIDI BADO TUNAKWEPA UKWELI!!!
Mdau Isack Mchungu

Ripoti ya mwaka 2009 toka Shirika la Umoja wa Mataifa la kupamba na Ukimwi duniani USAIDS inaonesha kuwa idadi ya watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi VVU duniani sasa imefikia milioni 33.4 Watu wazima milioni 31.3 wanawake ni milioni 15.7 na watoto chini ya miaka 15 ni milioni 2.1.

Watu waliopata maambuzi mapya ya VVU ni milioni 2.7 ambapo watu wazima ni milioni 2.3 huku 430,000 ni watoto chini ya miaka 15


Waliopoteza maisha yao kutokana na ugonjwa wa UKIMWI ni milioni 2 watu wazima ni milioni 1.7 na watoto chini ya miaka 15 ni 280,000

Eneo la Kusini mwa Jangwa la Sahara ndIo linabakia kuwa limeathIrika zaidi duniani kutokana na UKIMWI na VVU,Kwani eneo hili limeonesha kuwa na asilimia 67 ya maambukizo ya VVU duniani,asilimia 68 ikiwa ni maambukizo mapya kwa watu wazima na asilimia 91 kwa watoto.

Hali hii imesababisha kurudisha nyuma maendeleo ya kaya,jamii na nyanja mbalimbali za uchumi na kiroho katika eneo hili.

Taarifa hiyo pia inaonesha kuwa idadi ya watu wanaoishi na VVU kusini mwa jangwa la sahara ni milioni 22.4 watu waliopata pata maambukizo mapya ni milioni 1.9 ambapo watoto walipata maambukizo ya VVU ni 390,000 na watu milioni 1.4 wakiwa wamepoteza maisha yao.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.