MTANGAZAJI

IVORY COAST KUWEKA KAMBI TANZANIA

Timu ya soka ya Ivory Coast

Miongoni mwa habari za michezo zilizopewa kipaumbele na vyombo mbalimbali vya habari hapa nchini toka jana jioni ni ujio wa timu ya soka ya Taifa ya Ivory Coast.
Timu hiyo ambayo ni miongoni mwa timu sita toka barani afrika zitakazocheza kombe la dunia mwakani huko Afrika Kusini itawasili Januari 2 na kuweka kambi ya wiki moja kabla ya kuelekea nchi Angola kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika mwakani.

Mashabiki wa Tanzania watapata nafasi ya kuwaona wachezaji wa timu hiyo wanaocheza barani Ulaya akiwemo mshambuliaji wa kimataifa wa timu hiyo anayekipiga na klabu ya Chelsea, Didier Drogba.

Taifa Stars na Ivory Coast zitashuka dimbani Januari 4 na Januari 7 ambapo Stars itatumia fursa hiyo kujiandaa na michuano ya mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN).
Mtazamo News . Powered by Blogger.