TANZANIA HAKUNA WASANII???
Ndugu zangu leo nilitembelea kariakoo na baadhi ya maeneo ya Kinondoni pamoja na Temeke kuona jinsi kazi za wasanii zinavyoibiwa washiriki wakuiba kazi hizi pamoja na wadau wengine wengi wanaohusika na shuguliza sanaa kwa ujumla ,.
Nilivyofika Kariakoo kwanza nilishangaa nilipoambiwa Msanii Ali Kiba amepeleka nyimbo yake moja inayobeba Jinala album yake mpya hapo sehemu akapewa alfu 20 akaishia zake.
Wasanii wengi sana nao huwa wanapeleka singo zao sehemu hiyo kwa bei che huyo jamaa kazi yake ni kuchanganya nyimbo hizo na kutengeneza CD moja ambayo inauzwa kama njugu hawa wezi wengine wa sanaa hizi huwa wanachukuwa toka eneo hilo hilo nao wanauziwa kwa bei ndogo au wanachukuwa kiurafiki tu.
Ukienda maeneo ya temeke nako ni hivyo hivyowasanii kupeleka nyimbo zao wenyewe bila wasimamizi wao kujua ---
Kwaupande wa watengeneza miziki hii nao wanakosa moja kwa sababu hizi kazi zinatengenezwa kwao kwanini wao wasiweze kulinda kazi za wasaniiwanaofanya kazi kwao pamoja na kuwapa mikataba ambayo inatekelezeka ?
Hili halishindikani mimi sio mtaalamu wa masuala ya miziki au biashara hii lakini naona linawezekana lakini na wao pia wanaongoza katikak utumia programu bandia kwenye shuguli zao za kila siku ( pirated ).
Kama askari wakiamua kusaka programu bandia kwenye studio za muzikinakwambia wengi wataumbuka au kufunga studio zao kwa pesawatakazotakiwa kulipa kama faini na vifungo juu.
Kuna mfano mmoja miezi michache iliyopita nchini Afrika ya Kusini mmoja wa wasanii maarufu katika nchi hiyo alitengeneza nyimbo ambayo ilikuwa inafanana na moja ya JAYZ hata kwenye kasha la album yake alipiga picha inayofanana kidogo na album mpya ya JAYZ alifikishwa kwenye vyombo husika wasambazaji wote wa kazi zake wakaondoa kazi zake kwenye maduka yao ya kuuza kazi hiyo .
Hapa kwetu msanii TID aliwahi kuiga nyimbo ya mwanamuziki mmoja wa Msumbiji , nyimbo hii mpaka leo bado inapigwa kwenye radio mbalimbalinchini mpaka kuonyeshwa kwenye matifii yetu .kilichofanyika afrika kusini hapa kinawezekana.
Yona F.Maro

Post a Comment