SIKU YA UKIMWI DUNIANI 2009
JE UMETIMIZA WAJIBU WAKO?
Mosi: Elimu ambayo ilitakiwa kutolewa kwa wananchi, kubainisha UKIMWIni nini, kisayansi, haijawahi kutolewa hata siku moja. Kumekuwa namkazo wa kuupiga vita UKIMWI lakini bila ya kuwaelimisha watu kwaufasaha wanaupiga vita kwa sababu gani. Asilimia kubwa ya ujumbe ambaoumeenezwa kwa wananchi ni kwamba kiwango kikubwa cha maambukizo ya VVUhupatikana kwa njia ya kujamiiana, hivyo, watu wanapaswa kutumia kingawakati wote wa kujamiiana.
Haikuwahi kutolewa elimu kuwaeleza wananchiUKIMWI ni nini, jinsi mtu anavyoweza kuambukizwa, VVU vikoje, nakadhalika. Hakukuwahi kuwapo na mpango wa kisayansi wa kuwaelimishawananchi kwa ufasaha, UKIMWI ni nini.
Kama kungekuwapo na mpango wakisayanzi wa kuwaelimisha wananchi kwa ufasaha UKIMWI ni nini na namnaya kuupiga vita, tusingelazimika kuendesha kampeni ya kitaifa yakupima VVU, kwani, watu wangekuwa wakimiminika wenyewe kwenye vituovya ushauri nasaha na kupima endapo wameambukizwa VVU kwa hiari yaowenyewe! Kama elimu hiyo ingekuwepo, Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania asingelazimika kuwa Mhamasishaji Mkuu wa kampeni hii.
Kama...lakini elimu hiyo haikuwepo, haijakuwepo, na nina uhakika kwambaasilimia kubwa ya wajumbe waliopo kwenye kamati hiyo walikuwa namajukumu ya kutayarisha na kutekeleza mikakati ya elimu hiyo, kitaifa,jambo ambalo halikufanyika. Mpango huo, kwa uwajibikaji, ulikuwa chiniya Mpango wa Taifa wa Kudhibiti UKIMWI (NACP), lakini haukutekelezwa.
Mpango wa Elimu ya UKIMWI kwa Umma (National Public AIDS AwarenessEducational Campaign) haukuandaliwa wala kutekelezwa. NACP walikuwawapi?Pili: Vita ambayo imekuwa ikipiganiwa juu ya UKIMWI imekuwa kujikingana UKIMWI, sio kuwaelimisha wananchi – ambao ndio askari muhimu katikavita hii kali – kwamba unapoambukizwa VVU sio mwisho wa maisha yako.
Kumekuwa na matukio mbali mbali ya kuwabagua, kuwanyanyasa nakuwatenga watu ambao wameambukizwa VVU, kiasi kwamba hofu kubwaimetanda miongoni mwetu. Watu wameshuhudia – wanaobisha wamwulize Dk.Sebastian Ndege, anayeendesha kipindi cha redio cha “Njia Panda”kwenye kituo binafsi cha redio cha Clouds FM – jinsi ambavyo watuwalioambukizwa VVU wamekuwa wakitengwa, hata na ndugu zao! Watuwameshuhudia jinsi wazazi walivyowatenga vijana wao, wake kwa waume,kwa “kosa” la kuambukizwa VVU. Watu wameshuhudia jinsi ambavyo jamii“imewatenga” na “kuwazika wakiwa hai” watu ambao wameambukizwa VVU,kiasi ambacho hofu kubwa imejengeka miongoni mwetu.
Hofu hiiimesababisha watu kuogopa, ama kwenda kupima VVU kwa kuhofia kupatamajibu “mabaya”, au kujitangaza pale ambapo wanapobaini kuambukizwaVVU, kwa kuhofia “kutengwa” na “kuhesabiwa kuwa wamekufa”, huku,pengine, bado wangeweza kuwa na maisha mazuri, ya kawaida, kwa miakakadhaa. Hofu hii imechangia kwa kiasi kikubwa kuongeza kiwango chamaambukizi kutokana na kwamba, watu ambao tayari wameambukizwa nahawajui kama wameambukizwa wamekuwa wakiendelea kujamiiana na watuwengine ambao hawajaambukizwa, bila kupima afya zao.
Watu hawawamekataa kupima kutokana na woga, woga wa kutengwa, kunyanyaswa nakubaguliwa na wenzao katika jamii.Tatu: Pengine, itastaajabisha, jambo ambalo limewekewa mkazo mkubwazaidi, yaani, matumizi ya kinga – kondomu – dhidi ya UKIMWI, nalo pialimekumbwa na utata. Tumekuwa tukipata ripoti kadhaa juu ya kukosekanakwa “silaha” hizi muhimu, kiasi kwamba kuna sehemu kadhaa ambapo watuwamekuwa “wakiwakodisha” watu wanaotaka kujamiiana “silaha” hiziambazo tayari zimekwishatumika, na hazifai kutumika tena, ili kwendakuzitumia katika kupambana na UKIMWI.
Inaweza kuonekana kama mzaha,lakini, kuna baadhi ya vijiji ambavyo viko mbali, havifikiwi mara kwamara na watendaji husika, jambo ambalo limewafanya wananchi wanaoishikwenye maeneo hayo kujihisi kwamba, labda, vita hiyo haiwagusi wao, nawala wao hawahusiki na vita hiyo. Huu sio mwelekeo sahihi.
Ni ajabu,lakini hata baada ya vyombo vya habari kueleza kwa kina tatizo hili lauhaba mkubwa wa “silaha” za kupambana na UKIMWI, yaani kondomu, kwenyemaeneo hayo ambayo hayafikiwi kwa haraka kwa sababu ya kutokuwapomiundombinu sahihi kama vile barabara, vyombo vilivyopewa dhamana yakupigana vita hii vimelipuuzia tatizo hili.
Wananchi wanaoishi sehemuhizo wameendelea kutumia “vifanyio” kwa kukodishana, jambo ambalo nidhahiri limechangia kasi ya maambukizi mapya ya VVU.
Jambo lingine ambalo limechangia kwa kiasi kikubwa Watanzania kupatamaambukizo ya VVU kwa kiwango kikubwa ni dhana potofu juu ya UKIMWI.Leo hii, UKIMWI unaonekana kuwa ni malipo ya “dhambi” ya zinaa. Kwakiwango kikubwa, Watanzania wanauchukulia UKIMWI kwamba ni malipo kwawatu wanaofanya zinaa, huku wakisahau kwamba, mosi, kuna vijana wadogokabisa wanaosoma shule za msingi, sekondari na haya kwenye vyuo vyajuu, ambao wameambukizwa VVU tokea wakiwa tumboni mwa mama zao.
Wapopia walioambukizwa wakati wakinyonyeshwa maziwa na mama zao. Je, nahao pia walifanya zinaa, kwa hiyo wanastahili “adhabu” hiyo? Je, nawale ambao waliambulikizwa VVU kwa kuchomwa sindano ambazo hazikuwasafi, kwenye zahanati za mitaani ambazo hazizingatii kanuni bora zaafya?
Je, na hao pia wana “dhambi”, ndio wastahili “adhabu” hiyo?Mtazamo huo potofu, wa kuufanya UKIMWI kuwa ugonjwa wa “ajabu” na wakuogopwa, na wa kumhukumu kila ambaye ameambukizwa VVU kuwa “mhalifu”ni jambo ambalo limechangia, kwa kiwango kikubwa sana, kwa watukuendelea na hamsini zao bila kujali kwenda kupima kama wameambukizwa,na wale ambao wameambukizwa kuendelea na vitendo vya ngono bilakutumia kinga, hivyo kuendelea kuwaambukiza watu wengine bila ya waowenyewe kujua.
Pia, kuna watu ambao wanafahamika – kwa ushahidi wa mazingira – kwambawameambukizwa VVU, lakini kutokana na utajiri wao, haswa kwa wanaume,wamekuwa “wakibadilisha” wanawake kama wanavyobadilisha mashati yao.Watu hawa, tena kwa makusudi kabisa, wamekuwa wakitumia “visu” vyaokutembea na wasichana wadogo wadogo, na kuwaambukiza VVU, kwa kuwapazawadi zenye thamani kubwa pamoja na kuwastarehesha.
Kuna waliodirikihata kuwachukua wasichana hao wadogo wadogo na kwenda kustarehe naonchi za nje, kisha kuwazawadia vitu vya thamani kubwa, kama vilemagari madogo aina ya “baloon”, au simu za mkononi zenye thamanikubwa. Kutokana na tamaa zao, wasichana wadogo wamekuwa wakibabaikakila wanapowaona wenzao wakipewa zawadi hizo, hivyo kujirahisisha kwa“wazito” hao, wakisababisha kukua kwa mtandao wa maambukizi mapya yaVVU.
Sasa mtaniuliza: Nini kifanyike?Wote tunajua kwamba, unapokwenda vitani, lazima kwanza ufanye utafitikumjua kwa undani adui yako. Lazima umjue yeye ni nani, marafiki auwashirika wake ni nani, anaishi wapi, ana fikra gani, mbinu zake zakivita ni zipi, ikiwezekana, ujue kila anachofanya kwa muda wote, ilikuweza kujua ni wakati upi utakaokuwa sahihi kumvamia na kumpiga bilaya yeye kuweza kujipanga. Hizi ni mbinu za kijeshi ambazo hufanywa nawanajeshi wote duniani, kabla ya kwenda vitani.
Kumchunguza adui yakouweze kufahamu udhaifu wake.Tumeingia kwenye vita dhidi ya adui UKIMWI bila kumjua kwa undani aduiyetu. Hatujamchunguza, yeye ni nani, marafiki au washirika wake ninani, anaishi wapi, ana fikra gani, mbinu zake za kivita ni zipi, nahatujajua ni wakati gani muafaka wa kumshambulia ili asiweze kujipangana kujibu mashambulizi yetu.
Tumekwenda kumpiga vita adui UKIMWI bilaya kuwa na dira, bila ya kuwa na mpango, tumepoteza muda mwingi nafedha nyingi, huku askari wetu wengi wakiteketezwa na adui huyu. Badotunataka kuendelea na vita hii?Mimi ninawasifu sana watu wa Uganda, kwani, wakati UKIMWIulipogunduliwa, vijana wengi sana – wanafunzi wa shule za msingi,sekondari na vyuo – walipukutika kama majani, kwa vifovilivyosababishwa na UKIMWI. Vilio vilitanda kila kona ya nchi yaUganda, sio mijini pekee bali hata vijijini.
Wananchi wa Uganda wakashtuka, wakasema: Hapana! Tutajipanga upya!Mikakati ya kuwafundisha wananchi, kuanzia ngazi ya kijiji, kuufahamuUKIMWI, kwa undani wake, ilifanyika. Watu wakafahamu UKIMWI ni nini,wakabadilika kitabia na kifikra. Wakaacha kuwabagua, kuwanyanyasa nakuwatenga watu wengine walioambukizwa UKIMWI.
UKIMWI ukaonekana kuwaugonjwa wa kawaida tu!Hilo ndilo jambo la msingi – kuufanya UKIMWI uonekane kuwa ugonjwa wakawaida tu! Hapo, ubaguzi uliisha, kutengwa kukakoma, na hakukuwa navitendo vya kuwanyanyasa watu walioambukizwa UKIMWI. Kila mtualiendelea na shughuli zake za kawaida, lakini kwa makini zaidi.
Watuwalikwenda kupima UKIMWI kila mara, bila ya kuwa na hofu wala woga,wakijua kwamba, kama walikuwa wameambukizwa, wangeendelea kuishi bilamatatizo yoyote. Hali ilikuwa shwari.
Ukichunguza takwimu zamaambukizi ya UKIMWI nchini Uganda leo, katika nchi zote za AfrikaMashariki, Uganda ina maambukizi mapya machache kuliko nchi zote zaAfrika Mashariki. Uganda imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kwenye vitadhidi ya UKIMWI.Tujiulize.
Kinachotutofautisha sisi, Watanzania, na wenzetu, majiranizetu, Waganda, ni kipi? Kwa nini wao waweze kufanikiwa kwa kiwangokikubwa huku sisi tukiwa watazamaji? Kwa nini sisi hatutakikubadilika?Tunaweza kubadilika, na tunaweza kufanikiwa, iwapo tutaweka mikakatithabiti, ya, kwanza, kuyajua yote ambayo tunapaswa kuyajua juu yaUKIMWI.
Tunao madaktari, ambao wanaweza kushirikiana na wataalamu wa sekta yateknolojia ya habari na mawasiliano (TEKNOHAMA), kutayarisha makalakwenye magazeti na majarida, pamoja na vipindi maalum ambavyovitaoneshwa kwenye luninga au kutangazwa kwenye redio.
Vyombo vyahabari vina nafasi kubwa na muhimu ya kutoa mchango wa elimu katikavita dhidi ya UKIMWI, kupitia majarida na magazeti, vipeperushi,mabango, luninga, redio, na pia, wasanii wa fani mbali mbali, kamavile fasihi simulizi na fasihi maandishi.
Kwenye fasihi simulizi kunatamthilia (maigizo, nyimbo, ngoma za jadi, n.k.) wakati kwenye fasihimaandishi kuna viandiko (majarida, magazeti, vitabu, mabango,vipeperushi, n.k.).
Kama ikibidi, wasanii wa maigizo kwenye luningawalipwe – chini ya mpango maalum wa dharura – ili waweze kutungamichezo ya kuingiza itakayowaelimisha watu juu ya UKIMWI, namnaambavyo mtu anaweza kuambukizwa VVU, jinsi ambavyo mtu anawezakujikinga dhidi ya maambukizo, na kadhalika. Mchango wa vyombo vyahabari tayari umeonekana, kwa mfano, mpango wa kitaifa ambao umekuwaendelevu, katika kuelimisha na kuchangia vita dhidi ya sarataniinayowaathiri wanawake (kwa uwingi wao) na hata wanaume (kwa uchachewao).
Mchango mkubwa ambao umekuwa ukitolewa kwa Chama cha MadaktariWanawake wa Tanzania (MEWATA) usingefanikiwa kama vyombo vya habarivisingeshirikishwa kwenye kampeni hiyo.
Kampeni kama hiyo inaweza piakufanikiwa, katika vita dhidi ya UKIMWI, kama vyombo vya habarivingeshirikishwa ipasavyo. ITV na MEWATA wameonesha njia, TACAIDS naNACP wameiona?Wengi wetu hatujui “A” wala “B” kuhusu UKIMWI. Binafsi, ukiniulizakuna aina ngapi ya VVU sitaweza kukujibu.
Nenda sehemu yoyote yaUganda leo, waulize watoto wadogo, watakutajia aina zote za VVU. Ala?Hivi kuna zaidi ya aina moja ya VVU? Mlikuwa hamjui?Wataalam wa teknolojia ya habari na mawasiliano wako tayari kuandaavipindi maalum ambavyo vitawaelimisha wananchi kupitia luninga naredio, kinagaubaga, ili waweze kuujua UKIMWI.
Wasanii wataweza kuandaamichoro, kutokana na maelezo ya madaktari na wataalam wa afya, ilikuweza kuonesha mifano ya maumbile ya VVU. Katika kuelezea UKIMWI,kupitia mbinu za kisayansi, tutaweza kuujua UKIMWI na tutawezakuubomoa.
Hakuna elimu ya kutosha kwa sasa juu ya UKIMWI. Mpango wa Taifa waKudhibiti UKIMWI, katika miaka yake yote tokea ulipoanzishwa,haujaandaa kipindi hata kimoja, ambacho kingerushwa kwenye luninga aukutangazwa kwenye redio, kuwaelimisha wananchi “kisayansi”, UKIMWI ninini.
Ninakumbuka, mwanzoni kabisa, mabango yaliyokuwa “yakielimisha”wananchi juu ya UKIMWI yalikuwa na michoro ya watu waliokondeana,wakionekana dhahiri kuwa na afya mbaya. Jambo hili liliwatisha watuwengi, ikaonekana ni makosa. Lakini ile dhana kwamba ukiambukizwaUKIMWI ndio mwisho wa maisha yako, kwa kusema “UKIMWI UNAUA” ilikuwatayari imejengeka.
Bado, kuna maandishi kadhaa kwenye machapisho mbalimbali, yanayosema “UKIMWI NI HATARI. UNAUA. JIHADHARI NA UKIMWI!”Machapisho haya yanawatisha watu, yanaogopesha, yanakwamisha vitadhidi ya UKIMWI!Kwa mtazamo wangu, lazima tukubali kwamba tulifanya makosa, na sasabado tuna nafasi ya kujirekebisha. Sisemi kwamba “tuurembe” UKIMWI kwakuufanya uonekane kwamba sio hatari. La hasha.
Tuwe na mtazamo kwambaunapoambukizwa sio mwisho wa safari ya maisha yako. Watu wanaoishi naVVU wana nafasi kubwa katika vita hii, kwani wao ni mfano tosha kwambaunaweza kuwa umeambukizwa lakini ukaendelea kuishi maisha ya kawaida.Wao ndio walimu wetu katika vita hii, tuwape nafasi ya kutuelimisha.
Hata hivyo, licha ya kukubali kwamba kuambukizwa UKIMWI sio mwisho wamaisha, hakuna maana kwamba tuache kujikinga na kuwa makini wakatiwote. La hasha. Tunatakiwa tuongeze bidii katika vita hii.
Ninampongeza Rais Jakaya Mrisho Kikwete kwa kusimama kidete nakuwashauri wananchi kwenda kupima UKIMWI. Nimewahi kupima UKIMWI nanitapima tena siku hiyo. Nitayakubali matokeo yoyote yale. Kwanikuambukizwa UKIMWI sio mwisho wa maisha yangu.Lakini tukumbuke:
Je, tumejipanga vizuri katika vita hii kubwa kuliko zote?
Abdalah Hamis
Leo ni siku ya Ukimwi duniani. Ulipoamka leo watu zaidi wameambukizwa
UkimwiPamoja na ukweli kuwa gonjwa hili linatumaliza mmoja baada yamwingine, inaaminika kuwa kuna baadhi yetu ambao bado wana ule mtazamo wa "ajali kazini."
Na wengine wanasema, "Kama ni kufa, binadamu wotetutakufa." Ukimwi ni hatari, tukubali au tukatae. Ni watu wachachesana hivi sasa katika nchi za Kusini mwa Afrika ambao hawafahamu mtuau watu ambao wana Ukimwi au wameshakufa kwa Ukimwi.
Mimi mwenyewekijijini kwetu nimeshaacha kuhesabu siku nyingi. Sitanii.
Sio ndugu,majirani, marafiki, n.k.
Wakati tunakumbuka siku hii ya Ukimwi Duniani, tusisahau kuwa Malariabado ni ugonjwa unaoua watu wengi zaidi ya ugonjwa wowote duniani.
Tutumie siku hii kukumbuka ndugu zetu, marafiki, majirani, wafanyakaziwenzetu walioaga dunia na wapendwa wao walioachwa duniani. Pia tutumiesiku hii kuamua kuishi kwa usalama na wajibu-binafsi maana uhai wakotunauhitaji sana. Mapambano bado hayajaanza.
YONA F.MARO
Kuna mambo kadhaa lazima tuyatazame kwa undani.
Moja: vitendo vya ngono nje ya ndoa au kabla ya wakati vimekuwepoduniani kabla ya kondomu. Ziwepo kondomu au zisiwepo vitafanyika.Ukienda kwenye jamii ambazo hazijui kitu kiitwacho kondomu (na zikonyingi duniani) utakuta vitendo vya ngono viko juu sawa na jamiiambazo wanatumia kondomu.Tunaweza tusipende iwe hivi ila ndivyo ilivyo. Hiyo ni moja.
Mbili: hakuna siku ambayo tutaishi kwenye dunia ambayo vijana na hatawazee wataacha kufanya vitendo hivo nje ya ndoa au kabla ya wakati.
Tatu: wako watu ambao wataitikia wito wa kuacha vitendo hivyo ilakutokana na ukweli niliousema katika namba mbili, wako watu ambaohawatasikia (iwe ni kampeni za serikali, mashirika, au mafundisho yadini).
Swali kuu ni hili: je watu hawa ambao tunajua fika kuwa wataendeleakufanya vitendo hivi kama ambavyo imekuwa ififanywa miaka maelfu namaelfu tukitakiwa kuwashauri tuwaambie nini? (kumbuka: ninazungumziawale ambao hawataacha kwahiyo ushauri wa "acha zinaa" ni kupotezamuda).
Wanatakiwa washauriwe vipi ili kulinda nguvu kazi na vizazivijavyo?Kumbuka kuwa kundi hili ni wengi.Kwahiyo utaona kuwa ujumbe kama wako au wa viongozi wa dini kuhusukuacha kabisa vitendo hivi unafaa maana kuna watu ambao wataitikia.Lakini swali kuu kwangu sio kuhusu watu hao bali ni wale ambaohawatasikia. Ambao wako...tena wengi.
Khadija Abdul Razak

Post a Comment