MTANGAZAJI

MAISHA BORA KWA WATANZANIA???!!!!

Unaweza ukadhani hapa ni Darfur nchini Sudan lakini ukweli hili ni eneo la makazi katikati ya jiji la Dar es Salaam lilipo eneo la Chang’ombe, wilayani Temeke.
Wakazi wa eneo hili wamekuwa wakiishi maisha duni baada eneo hilo kuchukuliwa na mwekezaji mmoja na pesa zao za fidia zilizotolewa awali na mwekezaji huyo kutafunwa na vigogo hali iliyosababisha wakazi wa eneo hilo na mwekezaji kuwa katika mgogoro mkubwa. Sakata hilo limedumu kwa zaidi ya miaka kumi na tisa sasa.
Mbali na kuishi maisha duni wakazi hao pia wapo katika eneo la hatari kwani wamezungukwa na matanki ya mafuta ya Petroli pamoja na kemikali zinazotoka katika viwanda vinavyozunguka eneo hilo.

Naomba maoni yenu kutokana na Falsafa ya Chama Chetu kilichoshika hatamu za uongozi wa nchi yetu.
Mdau Sylvanus Kessy

1 comment

Born 2 Suffer said...

Hii ni kila sehemu bro si TZ tu nchi tajiri na za kiarabu wapo watu wanaishi kama hivi.

Mtazamo News . Powered by Blogger.