UNAFAHAMU KINACHOBEBWA NA WANAFUNZI KWENYE MABEGI?
Kumekuwa na tetesi kuwa baadhi ya wanafunzi wa shule za msingi na sekondari hapa nchini wamekuwa wakibeba vitu ambavyo hawapaswi kuvibeba kwenye mabegi yao wakati wakienda ama wakitoka shule hasa wake wanaosoma katika shule ambazo si za bweni.
Kwa muda mrefu blog hii imefanya utafiti kwa kuzungumza na watu wazima mbalimbali na wanafunzi pia na imeonekana kuna tatizo kubwa ambalo hata wazazi walimu hawafahamu kinachoendelea jambo ambalo ni hatari kwa maendeleo ya wanafunzi na maisha yao kwa ujumla.
Imegundulika kwamba baadhi ya wanafunzi wa kike hutoka nyumbani wakiwa wamevaa sare za shule na wakifika mahali fulani ambapo hawaonekani na watu ama mahali ambapo kuna sehemu ya kujisetiri basi hubadilisha nguo kwa kuvaa nguo za nyumbani ambazo huwa wamebeba kwenye mabegi na hivyo huelekea kwenda kufanya ngono ama mambo yanayofanana na hayo.
Wanafunzi hawa hukaa katika sehemu ama nyumbani kwa watu walio na uhusiano nao mpaka itakapofika muda wa kurudi nyumbani kwa wanafunzi ambapo hubadilisha nguo na kuvaa za sare za shule tena na huonekana kuwa wanatoka shule kumbe si hivyo.
Blog hii ilishuhudia hivi karibu mwanafunzi wa shule ya sekondari mojawapo hapa Morogoro nyakati za jioni akiwa maeneo ambayo si shuleni na nguo za nyumbani na ndipo alipoingia eneo lililojificha na kubadilisha nguo na kuvaa sare za shule na akarudi nyumbani hali hiiyo ilinistua ndipo nilipoamua kufuatilia na kuambiwa kuwa baadhi ya wanafunzi wa kike ambao wanaacha kwenda shule na kwenda kufanya ngono wamekuwa wakifanya ujanja huo kwa ajili ya kukwepa kuonekana na sare za shule.
Dada mmoja ambaye ni mzazi nilipomwuliza alisema tabia hii ipo sana miongoni mwa wanafunzi wa kike, JE WAZAZI,WALEZI NA WALIMU WANALIFAHAMU HILI????
Post a Comment