MTANGAZAJI

LUSAKA,ZAMBIA

Hapa niko na mwandishi wa habari wa siku nyingi nchini Tanzania ambaye kwa sasa yuko Redio Uhuru Dar es saalam,Deogratius Kiduduye hapa tukiwa tunajiandaa kuingia katika mjadala wa Mazingira ulioendeshwa na Baraza la Mazingira la Zambia,waandishi wa habari wa Zambia na wadau wa mazingira nchini humo.

Hivi karibuni nilibahatika kuhudhuria mafunzo ya wiki mbili ya uandishi wa habari huko Lusaka,Zambia.Mafunzo hayo yaliyoendeshwa na NSJ ambayo yalihusu "Communication for Social Change"na kufanyika katika Hotel ya Longacres yaliwakutanisha waandishi wa habari 14 toka Tanzania,Zambia,Malawi,Lesotho,Botswana,DRC,Msumbiji na Zimbabwe.Katika picha hii niko na Mtangazaji wa Televisheni ya Malawi Dada Milly na Mwandishi wa habari wa Shirika la habari la Zambia,Mishack Moyo,wanahabari hawa walinipa changamoto sana ya utendaji wa kazi katika taaluma hii ambayo inachangamoto kubwa kutokana na mabadiliko yanayotokea kila siku maishani

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.