MTANGAZAJI

TONY ONDITI

Tony Onditi wa kwanza kushoto akiwa na kundi la The Pilgrims huko Uingereza wengine ni Singo,Fredy Manento,Kim Matinyi,Ezekiel Mkundi na Jack Ndugu


Darlington Onditi akifundisha waimbaji wa Kirumba Adventist Choir ya Mwanza mwaka 2006





Darlington Onditi akiimba moja ya nyimbo zake katika kanisa la waadventista,Kirumba Mwanza mwishoni mwa mwaka 2006 alipokuwa likizo





Amekuwa mwimbaji na mwalimu wa kwaya za muziki wa injili hapa Tanzania na nchi za nje kwa muda usiopungua miaka 25 huyu si mwingine bali ni Darlington Onditi.Ingawa maendeleo yake hayakuja kwa bahati bali ni kutokana na juhudi zake za makusudi katika kuhakikisha kuwa anafikia malengo yake kimuziki.

Tony kama anavyojulikana na wengi akitokea mjini Mwanza kwa sasa yuko masomoni nchini Uingereza ambapo anaimba katika kundi la The Pilgrims linaloundwa na watanzania sita na pia akiifundisha kwaya ya kanisa la waadventista la Whitley.

Mwanamuziki huyu anaeleza kuwa pamoja na juhudi zake binafsi maendeleo yake yaliwekewa msingi na waimbaji na walimu wa muziki wa injili wa kiadventista hapa Tanzania ambao ni Josia Sagati,Patroba Maginga na James Gayo(Kingo) ambao alikutana nao katika kwaya ya kanisa la waadventista,Kirumba,Mwanza baada ya kumaliza kidato cha nne,mwaka 1985.

Akiwa nchini Uingereza ameshatoa albamu mbili ambazo amemshirikisha mtayarishaji wa muziki wa injili na video Tegemea Champanda katika kutengeneza muziki,baadhi ya nyimbo katika albamu hizo ni "wimbo moyoni","God is love","Pendo la Mungu"na Redeemed"

Tony ambaye ameshahitimu shahada ya technolojia ya muziki na akikamilisha masomo yake ya shahada ya udaktari wa falsafa ya uongozi anataji kutoa vitabu viwili cha Kiongozi wa kwaya na uimbaji na mwimbaji ambavyo vitakuwa ni mchango wake katika kuendeleza muziki wa injili hapa Tanzania.

NINAMTAKIA MAFANIKIO













No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.