MTANGAZAJI

VIDEO YA THE VOICE WAKIWA UINGEREZA

Huenda umekuwa ukijiuliza kuwa kundi linalokuja kwa kasi katika muziki wa injili ambao umeanza kujipatia umaarufu hapa nchini kutokana na aina ya uimbaji wa kutotumia vyombo vya muziki, unaojulikana kwa jina la a cappela ni kundi mahili la The Voice lenye maskani yake jijini Dar es salaam lilianza vipi hapa Tanzania?

Kundi hilo linaloundwa na waimbaji watano kati yao wanne wakiwa ni ndugu ambao ni Obedi John Mark,Mark John Mark,Daniel John Mark,Baraka John Mark na Msafiri Simon Nicolaus aliyeko Uingereza ambaye nafasi yake imechukuliwa na Eliud Kweba. Halikuja kama bahati bali lilianzishwa hapa Morogoro na ndugu hao wanne mwaka 1996/1997 wakati huo wakiwa wanafunzi wa shule ya msingi na pia wanachama katika chama cha vijana wadogo wa kanisa la waadventista wanaojulikana kwa jina la Watafuta njia.

Kwa mara ya kwanza walisikika katika matangazo ya AWR kwenye kipindi cha watoto wetu ambapo nilifanya nao mahojiano nyumbani Forest Hill hapa Morogoro.Ambapo wakati huo walipenda sana kuimba wimbo wa Habari njema ambao umeimbwa pia na kundi la Royal Advent la mjini Morogoro.

Kutokana na baba yao mzazi kuhamishia maskani yake Dar es salaam,The Voice nao waliamua kuwafuata wazazi wao jijini na waliendelea kuimbaji katika kanisa la Waadventista Magomeni na sehemu mbalimbali ndni na nje ya Tanzania.

Mwaka 2006 ulifungua ukurasa mwingine kwa The Voice ambao kaka yao mkubwa anayejulikana kwa jina la Somi ambaye ni mpiga kinanda,kwani walipata mwaliko wa kwenda nchini Uingereza kwenye mahubiri yaliyoandaliwa na Kanisa la Angaza lililoanzishwa na baadhi ya watanzania walioko nchini humo,katika mkutano huo walioongozana na Mwinjilisti Mkangara toka Dar,wakiwa huko ujumbe wa nyimbo uliwagusa sana wasikilizaji.The Voice lilikuwa ni kundi la tatu la uimbaji wa nyimbo za injili za a cappella linalojumuisha waimbaji wa kiume kuarikwa na Angaza ,waimbaji wengine waliwahi kwenda huko ni Royal Advent Quartet(2004) na Magomeni Heralds(2005),mpaka sasa The Voice wana albamu mbili ambazo kwa kweli zinagusa wasikilizaji wa AWR na Morning Star 105.3 FM jijini Dar es salaam.

Waweza kuona video za nyimbo zao wakiwa nchini uingereza kwa kubofya katika linki hii iliyotayarishwa na mwanahabari mwenzagu aliyeko Uingereza Donald Bituro aliyekuwa shuhuda kwenye mkutano huo wa mahubiri yaliyoandaliwa na Kanisa la Angaza lililoko Reading,Uingereza:

http://www.youtube.com/view_play_list?p=479F4D01A9163B8F

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.