MTANGAZAJI

MCH.ISRAEL KAGYA ASIMIKWA KATIKA KANISA LA HOUSTON




Konferensi ya Texas ya Kanisa la Waadventista wa Sabato imemsimika rasmi Mchungaji Israel Kagya kuwa mchungaji wa Kanisa la Waadventista wa Sabato la Nations of Praise lililoko jijini Houston,Texas   Marekani katika ibada iliyofanyika kanisani hapo Septemba 7,mwaka huu.


Kagya anakuwa mchungaji wa Pili wa Nations of Praise baada ya Mch Matthew Makau ambaye alihamishwa miaka miwili iliyopita,na hii inamfanya Kagya kuwa Mchungaji wa kwanza aliyewekewa mikono kutoka Tanzania kuwa mchungaji katika wa Kanisa mahalia katika  Konferensi ya Texas na Mchungaji wa tatu kutoka Tanzania  katika miaka hivi karibuni kupata wito huo nchini Marekani.


Tovuti ya Konferensi ya Texas inaonesha kuwa ina zaidi ya makanisa ya Waadventista wa Sabato 300,yenye waumini 68,502 wanaotoka katika nchi zaidi ya 100,ambapo kanisa la Nations of Praise lililoanzishwa miaka minane iliyopita huwakutanisha waumini wa kanisa hilo wanaotoka katika ukanda wa Afrika Mashariki wanaoishi Marekani.


Mchungaji Kagya ambaye amewahi kuwa mchungaji wa Mtaa wa Liwale mkoani Lindi kwa miaka minne na Mtaa wa Ilala jijini Dar es salaam,Tanzania kwa miaka mitano Ana Shahada ya Kwanza ya Thiolojia na Dini kutoka Chuo Kikuu cha Arusha nchini Tanzania na kwa sasa anasoma  Shahada ya Uzamili ya Elimu ya Uungu, katika Chuo Kikuu cha Andrews,Michigan katika ujuzi uliojikita kwenye huduma za mijini, akilenga kushughulikia changamoto na fursa za kipekee zilizopo katika jamii za mijini.


Mchungaji Kagya amefunga ndoa na Esther Fadhili Mduma, mwenzi  wake katika maisha na imani. Ni wazazi wenye fahari wa mtoto wa kiume anayeitwa Nathaniel.



No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.