MWAKA 2023 WAWEKA REKODI KWA WAADVENTISTA
Uongozi wa Kanisa la Waadventista wa Sabato Ulimwenguni umeeleza kuwa idadi ya watu wanaojiunga na hilo imerejea kikamilifu baada ya changamoto zilizotokana na janga la COVID-19,.
Hii ni kwa mujibu wa David Trim, Mkurugenzi wa Ofisi ya Konferensi Kuu ya Kanisa hilo ulimwenguni inayohusiana na Kumbukumbu, Takwimu, na Utafiti.
Mwaka wa 2023, kanisa lilikaribisha washiriki wapya zaidi ya 1,465,000 zaidi ya 4,000 kwa siku, au mmoja kila sekunde 21.5. Mwaka 2023 ulishuhudia idadi kubwa zaidi ya washiriki wapya katika historia ya Kanisa la Waadventista.
Wakati huo huo, zaidi ya watu 836,000 waliacha kanisa hilo mwaka wa 2023 (bila kuhesabu vifo), ambayo ni idadi ya tatu kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa. “Hasara nne kubwa zaidi zimetokea katika miaka mitano iliyopita,” aliripoti Trim. Hivyo, aliongeza, “kujiunga pekee hakutoshi kwa ukuaji wa kanisa.
"Lazima tujipatie njia za kufunza washiriki zaidi ikiwa tunataka ukuaji wetu halisi uwe mkubwa zaidi.” Kwa sasa, asilimia ya washiriki wanaoondoka ni karibu asilimia 43, aliripoti.
Kuhusu uwiano wa washiriki Waadventista kwa idadi ya watu duniani, kwa sasa kuna Mwadventista mmoja kwa kila watu 350 ikilinganishwa na watu 519 kwa kila mshiriki wa kanisa mwaka wa 2000.
Post a Comment