MTANGAZAJI

MWANAFUNZI WA SEKONDARI AUA NA KUJERUHI WANAFUNZI WENZAKE

 


Moja wapo ya Tukio la kusikitisha lillilofunga mwezi Novemba  2021 nchini Marekani  ni la  Wanafunzi watatu kupoteza maisha  kwenye tukio la kupigwa risasi katika Shule ya Sekondari ya Oxford,huko Oxford Michigani ,jumanne Novemba 30,2021 mamlaka zimeeleza.

Waliopoteza maisha wametambuliwa kuwa ni Tate Myre (16), Hanna St. Julian (14) na  Madisyn Baldwin,(17).

Kwa mujibu wa Afisa wa Polisi wa Manispaa ya Oakland Mike Bouchard, wengine wanane walipigwa risasi na kujeruhiwa ikiwemo Mwalimu ambapo walisafirishwa katika hospitali tatu za mji huo,Watatu hali zao zilikuwa mbaya ikiwemo mvulana wa miaka 15 ambaye alipigwa risasi kichwani,msichana wa miaka 14 ambaye alipigwa risasi kifuani na kwa sasa anapumua kwa msaada wa mashine ya kupumulia na Msichana wa miaka 17 aliyepigwa risasi kifuani.

Mvulana wa miaka 14 naye hali yake ilikuwa mbaya akiwa na majeraha ya taya na kichwa,Wanafunzi watatu hali zao hazikuwa mbaya sana ikiwemo msichana wa miaka 17 na mvulana wa miaka 15,Mwalimu wa Kike mwenye miaka 47 alipata matibabu ya jeraha na kuruhusiwa kutoka hospitalini amesema Bouchard

 Mtuhumiwa wa tukio hilo ni mwanafunzi wa mwaka wa pili wa  kiume mwenye umri wa miaka 15, ambaye alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi kisha akanyang'anywa bunduki aliyokuwa akiitumia.

 Bouchard,amesema bunduki iliyotumika ilinunuliwa na Baba wa mtuhumiwa Nov 26,2021 na taarifa zinaonesha mtuhumiwa hivi karibuni aliweka picha kwenye mitandao ya kijamii akilenga shabaha kwa kinachoonekana kuwa alitumia bunduki hiyo.

Takwimu za Mtandao unaofuatilia matukio ya mauaji yatokanayo na bunduki nchini Marekani zinaonesha kuwa jumla ya vifo  20,625 vilitokea huku watu  40,090 wakijeruhiwa mwaka 2020 na mpaka kufikia Nov 21 mwaka huu jumla ya vifo 336 vimetoea na waliojeruhiwa ni 647.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.