MTANGAZAJI

WAZAZI WA MTUHUMIWA WA MAUAJI YA WANAFUNZI HUENDA WAKASHTAKIWA

 

Mwendesha mashtaka amerudia kuwatupia lawama wazazi wa mwanafunzi ambaye anatuhumiwa kuwaua wanafunzi wenzake huko Michigani,akiwaambia matendo yao yamekuwa ni uzembe uliopitiliza na maamuzi ya mashitaka huenda yakatoka ijumaa hii.

 “Wazazi  pekee ndio waliokuwa na nafasi ya kufahamu upatikanaji  wa silaha"Mwendesha mashitaka wa Manispaa ya Oakland Karen McDonald  amesema "Inaonekana ilikuwa huru kupatikana kwa mtu mwingine"

Ethan Crumbley(15), ameshitakiwa kama mtu mzima kwa makosa ya uhalifu ikiwemo mauaji,jaribio la kuua na ugaidi kwa kuwapiga risasi wanafunzi na mwalimu Jumanne ya Novemba 30 2021 katika Shule ye Sekondari ya Oxford,umbali wa Km 50 Kaskazini mwa Detroit,Michigani.

Wanafunzi wanne waliuawa na wengine saba kujeruhiwa,watatu wakiwa hospitalini na hali zao zinazidi kuimarika.

Kwa mujibu wa uchunguzi Bunduki aliyoitumia Ethan ilinunuliwa kihalali na Baba yake juma lililopita.

Wataalamu wanaeleza kuwa ni nadra wazazi nchini Marekani kusomewa mashitaka ya uhalifu wa kupiga risasi shuleni ukihusisha watoto wao Parents in the U.S. are rarely charged in school shootings involving their children, hata kama watoto watapa bunduki kutoka kwa  mzazi au jamaa nyumbani.

Hakuna sheria huko Michigani inayomtaka mmiliki wa bunduki kuwazuia watoto kuipata silaha hiyo,ingawa mwendesha mashitaka amependekeza kuna mengi ya kufanyika katika kesi hiyo.

Katika jimbo la Texas wazazi wa mwanafunzi ambaye alituhumiwa kuua watu 10 shuleni mwaka 2018 ameshtakiwa kwa kitendo cha mtoto kuitumia bunduki yake.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.