MTANGAZAJI

AFUNGWA KWA KOSA LA KUTAKATISHA FEDHA ZA MSAADA WA JANGA LA CORONA

 

 

Mwanamme katika jiji la  Houston ambaye alijipatia kwa udanganyifu Dola Milioni 1.6 za kimarekani kutoka kwa pesa za kujikimu wakati wa Janga la Corona, amehukumiwa kwenda jela kwa kosa la ulaghai na utakatishaji fedha.

Hakimu amemhukumu Lee Prince III(30) Jumatatu ya Novemba 30,2021  kifungo cha miezi 110 au miaka 9 na miezi miwili adhabu ambayo ataitumikia gerezani.

Prince alikiri kufanya kosa la wizi kwa njia ya utakatishaji fedha septemba 2021.

Waendesha mashtaka wa Serikali wanasema Prince alidanganya kwa taasisi mbili za fedha za mpango wa Serikali wa malipo ya fedha za kujikimu wakati wa Corona (PPP) ili ajipatie fedha hizo.

Moja ya maombi aliyowasilisha  ni kuwa na  kampuni ya Ujenzi yenye wafanyakazi 713 ambao miongoni mwao ni Afisa ambaye alishafariki mwezi mmoja kabla ya maombi hayo kuwasilishwa.

 Kwa mujibu wa mashtaka Price alipata Dola 700,000 kwa ajili ya kampuni moja na Dola 900,000 za  kampuni nyingine ambayo haikuwa na wafanyakazi.

 Alitumia Dola 200,000 kununua gari aina ya Lamborghini Urus, Ford F-350 pickup, Saa aina ya Rolex na vitu vingine vya anasa. Matumizi mengine ya gharama kubwa ni katika nyumba za starehe katika jiji la Houston.Mamlaka imeeleza kuwa wamekamata vitu pamoja na fedha vikiwa na thamani ya Dola 700,000

Serikali ya Marekani ilipitisha azimio la msaada wa dharula wa kiuchumi (CARES Act)  kwa mamilioni ya wananchi wake ambao wameathirika kiuchumi kutokana na janga la Corona nchini humo.

Baadhi ya watu na wafanyabishara ambao wanasifa na uhalali wa kupata fedha hizo wamelalamika kutozipata.

Tangu kuanzishwa kwa azimio hilo Kitengo cha serikali kinachohusika na Masuala ya Uchunguzi wa Udanganyifu wa fedha kimewafikisha mahakamani washitakiwa 150  katika kesi za jinai zaidi ya 95,ambapo wamekamata pesa taslimu Dola milioni 75,nyumba za kupangisha na vitu vya anasa.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.