MTANGAZAJI

TAHADHARI YA UTAPELI JIJINI DAR ES SALAAM

Naomba usaidie kuwasiliana na waandishi wengine ili kuelezea utapeli unaoendelea hapa mjini. Tayari watu watatu ninaowafahamu walitaka kutapeliwa kwa njia hii. Jamaa anakupigia simu na kujifanya anakufahamu sana. Anakuuliza kama bado unaishi Dar. Ukikosea ukisema ndio, anakueleza yeye yuko serengeti, na ana bosi wake ambaye ni procurement officer na  anamependekeza kwake jina lako ili ufanye nao biashara ya kununua vaccine za wanyama pori kwa ajili ya tiba. Ghafla anakuambia subiri uongee na boss. Bosi anakueleza jinsi walivyo na pesa nyingi kwa miaka 2 za kununulia madawa kutoka German.  Anataja vaccine anayoitaka haraka sana  inaitwa Gustavic animal vaccine 68f 1000mls - 50 pairs.

Anakulalamikia jinsi alivyofanya biashara na dr mmoja akawatapeli kwa hiyo wanakupendekeza wewe kwani huwezi kuwatapeli. Anakuambia mpigie dr huyo ambaye ni agent wa dawa hiyo umwulize bei. baada ya kupata bei anakuambia subiri accountant atakupia simu. huyo tapeli accountant akikupigia simu anakelezea jinsi walivyo na peasa na utalipwa cash kisha anakuunganisha na tapeli mzungu ambaye anakuambia uende haraka kusaini contract ya miaka 2 Double tree hotel masaki. Hapo sijajua ukifika watafanyaje kwani hawa jamaa zangu wamekuwa wakstuka kabla ya kufika double tree hoteli.
Inawezekana kuna watu wameshanaswa na hawa matapeli uchwala.
Source: www.wanabidii.net

16 comments

Anonymous said...

Asante sana kwa kutupa tahadhari juu ya wizi huu. Hata mimi nshawahi kupigiwa simu kuambiwa niende Ubungo kuchukua pesa niliyotumiwa kutoka Lushoto,lakini hata sipafahamu.

Anonymous said...

chakufurahisha zaidi mimi nasoma haya maelezo baada yakutoka kuongea na simu namutua ambaye anajifanya ni procurement officer na anahitaji kunitumia mimi kama middleman iliaweze kupata hii dawa, yeye yuko mara na boss wake yuko dar es salaam... ila nashukuru nimeona hii taarifa, mungu libariki taifa letu, mungu ibariki tanzania.

Yesu Anaokoa said...

Kweli Utapeli huu upo na umeingia Arusha pia kuna jamaa alijitambulisha kwangu kuwa ni james (Feki) na ananifahamu na siku hizi yuko mbuga za wanyama katavi kama store keeper, alidai kuwa maboss wake wa kizungu wako Arusha snow crest hotel walikuja kwenye mkutano wa wanyama pori na kuwa yeye alikuwa anatumiwa kuagiza hiyo dawa hapa arusha alikuwa akimtumia jamaa mmoja ambaye ni dr. msuya (Feki) kwa sasa hayuko amehamia south africa,sasa maboss wake wanatakiwa kununua hiyo dawa na kwasababu yeye alikuwa akila cha juu hakupenda maboss wake wafike kule dawa inakopatikana kwa hiyo akanipa no. ya dr. ibrahim (feki) ambaye anafanya na kampuni(feki) ya kuuza hayo madawa hivo akataka mimi niwe nafanya hiyo biashara badala ya dr.msuya (feki).
akanipa no ya dr. ibrahim (feki) nimuulize bei, kumpigia akadai kuwa dawa hiyo huuzwa kwa pair na kila pair ni tsh 850,000 wale wazungu walitaka pair 25.
Jamaa huyu tapeli james(feki) akaniambia kuwa atawapa wazungu no yangu watanipigia nijitambulishe na niwaambie mimi ni supplier mpya na niwaambie kwa pair ni sh1,250,000. wazungu feki waliponipigia wakadai kuwa watahitaji sample pair moja waone kuwa ni Genuine ndipo wanipe cash ya zote pair 25 nikawaletee zingine 24. dr. ibrahim feki akasema dawa pair ya sample haziwezi toka mpaka nilipie yaani sh 850,000 nikamuuliza ofisi zao ziko wapi akasema ziko njiro baada ya bp karibu na ABB (pale ni kiwandani na ni kiwanga cha madawa ya binadamu)
cha kushangaza wasivyo na Elimu dr. ibrahimu feki akasema nitume hizo pesa kwa Mpesa ili waanze kuandaa nikifika pale ziwe tayari kuanzai hapo nikashtuka.
WATU WAWE NA TAHADHARI. Hizi ni number zilizotumika:
James wa Katavi(feki): 0752491728
dr. ibrahim(feki): 0769979197
No ya MPESA: 0753692019

Anonymous said...

Its true guys,its happening to me right now thank god i remember about this post about matapeli.what should i do to them

Anonymous said...

nimegoggle baada ya kupigiwa simu na mtu akizungumzia hiyo dawa na mm nimsaidie kuipata kwa sababu maboss wake wanahitaji haraka. nashukuru nimesoma haya.
na bado anaendelea kunipigia cmu. Ngoja sasa apige asikie nitakachomwambia.

Anonymous said...

They tried to full me but they failed. watch out guys!

profesa said...

very helpful,sasa hivi nilikua nimepigiwa simu na mtu mmoja ambae anasema ananifahamu baada ya mazungumzo akanipigia mwingine nakuanza kuniambia nini natakiwa kufanya.kilichonishitua ni pale nilipotaka kuijua kiundani iyo vaccination yenye kupitia google..hapo ndipo nilipokutana na hii tahadhari nampaka sasahivi jamaa wananisubili niwajibu kama nimezungumza na dokta(hassani TPI NJIRO 0713 311 685).

Anonymous said...

nami nimepigiwa simu nikaambiwa na yule mtu mwenye vaccine mwenye, ambae anaitwa Dr. allen, kuwa nimtangulizie pesa kwanza kwa ajili ya packing ya kwenye ndege shilingi laki mbili na ishirini. nikamwambia jamaa yake mwenye dili kuwa anitumie hizo pesa kwa mpesa ili nimtumie huyo dokta kwani mi sina. ndo nasubiri baadae kidogo nimpigie picha liendelee. i want to get to the bottom of the matter.

Anonymous said...

jamaa mwenye dili anajiita Steven Mhagama wa serengeti (0762936911), jamaa mwenye mzigo anajiita Dr. Allan wa Agro Chemical, Mikocheni industrial area
(078865657), Accountant aliepo Double Tree anajiita Wanjiru Joseph Omondi (0756303124) anaongea kama mkenya.

Ukimtafuta steven mhagama huwezi kupata picha yake. utakuta alama za form four alizopata kwenye mtihani, na facebook profile ambayo inapicha ya ajabu ajabu enough to alarm any body.

Unknown said...

Mungu akujalie sana kwa kutufungua macho.

Leo kidogo ningeliwa pesa ya advance kwa ajili ya kutengeneza risit blank

Nimeshituka vitu viwili
1. Iweje mtu anunue mzigo wa bei kubwa na kulipa cash?
2. Iweje pesa ya risit itolewe kabla ya kukutana?

Cha msingi pesa ya haraka haraka ni mbaya.

Anonymous said...

Leo,nikiwa naiishi Moshi, nimepigiwa simu na mtu akijitamublisha kuwa ni rafiki wangu wa siku nyingi Saidi, akiwa sasa yupo Tanapa Serengenti(namba: 0755-809132) na Boss wake ana tenda atanipigia. Muda sio mrefu 'boss'wake Micheal (0767-060286 na pia kanipa namba 0716-918169)kuniambia nimpigie Dr Michael wa agrochemical
Dar, o763-609041 kumuiliza bei ya gustavic animal vaccine. Nilimpigie na kanipa bei ya Dollar 3,600/= kwa pair. Nilimpigia Boss Micheal na kumwambia bei.Akanijulisha kuwa tutawaambia wazungu Dollar 4,400 kwa pair na wapo Dar wakiwa wanatafuta hizo dawa.

Baada ya hapo,kuna mzungu kanipigia kuniuliza bei na nikamjibu bei 4,400/-! Halafu kaniuliza anataka serial namba ya mifuko special kusafirisha hizo dawa Serengti.Nikampigia boss micheal akanijibu itabidii ninunue hizo begi mbile kwa Tshs 300,000/-kila mmoja na kumpatia mzungu serial namba!Punde siyo mrefu, Dr Michael akanipigia na kunipa namba 0759-699061 (jina: Daniel Maningu) ilinitume Tshs 600,000/=!!
Siku zipeleka maana nikwaambia natumia ndugu yangu ambaye ni wakili huko Dar, na hawakunipigia tena?

Kwa taarifa zenu

Namba ya 'Saidi' mmiliki wa SIM hiyo ni Exaveri Kejeli

Namba za Boss Micheal;hazija sajiliwa!

Namba ya Dr Michael 0763-609041 mmiliki ni Freddy Josephat.

Namba ya kutuma mpesa ya Daniel Maningu 0759-699061 ni halali na kwa jina yake!

Jambo la kushangaza ni Saidi anajua majina zote za maduka zinazohusika na dawa za wanyama!Kwa hiyo pengine, hawa watapeli wako Moshi??

Unknown said...

yamenikuta hayo ila hawajapata ktu baada yakuniambia majina ambayo siyo sahihi,nlipowaambia majina yao wakaingia mitin

Anonymous said...

Huyo jamaa amenipigia sasa hivi, namba yake ya simu ni 0766 404810. Na mimi namzingua kama vile nimeingia mkenge, fala huyu nitamfunga.

Anonymous said...

Hahaha, mimi nimepigiwa simu jana na Bwana Cosmas Komba # 0756751471 akinishangaa kwa nini nimemsahau wakati tulikuwa wote mwezi wa saba Mbezi kwenye harusi ya binti yangu,aliniimbisha kuwa yeye ameniteua kuwa suplier wa vacine ya mifugo kwenye kampuni ya kizungu huko Serengeti.Alituma sms yenye namba ya Dr. Amos Mpacha #0789363477 nimuulize availability ya dawa GUSTAVIC LIQUID (best for animals) 68f, 1000mls made in German. Order ni 50 pairs Kwamba nimpigie nimuulize bei ya pair moja kwa wafugaji wadogo wadogo na wafugaji wakubwa ili tujue cha juu tunaongeza ngapi. Halafu nimwambie kuwa mimi ni rafiki wa Justin Masawe former supplier ambaye amekwenda masomoni ulaya hivyo anisaidie kunielekeza vizuri mimi bado mgeni wa mambo hayo. Dr. alionekana kumfahamu sana Masawe na kujitia kuniuliza mbona kapotea hajamuona muda,alinipa bei ambayo ni 3,000,000 per pair kwa wafugaji wadogo na 3,600,000 kwa wafugaji wakubwa na fedha ya packing ni 920,000 nilipompa taarifa hizo Cosmas akaniambia bosi wake mzungu atanipigia. Mara simu ikaingia #0684762257 jamaa akajitambulisha kuwa ni Mac Jenssen yuko Serengeti anahitaji Gustavic kwa ajili ya wanyama wa mbugani. Alijitahidi sana kuongea kama mzungu lakini mimi niligundua kuwa siyo maana wazungu wanajulikana wanavyoongea.mara akataka nimwambie bei zote na namba ya package. nikamrudia Dr. ambaye aliniambia nimtumie 900,000 kwenye simu yake ili awapelekee dahaco wapasue lile sanduku watakapowekea hizo dawa halafu atanipatia hiyo namba ili aipate mzungu. Nikamwambia sina hiyo hela kwa sasa hata mia sina. "Jitahidi Madam japo laki mbili umpe Dr. Masawe maana hatuwezi kukoza hela kubwa kama hiyo kizembe. mimi niko radhi kumpa 2m huyo atakayekukopesha laki 9 kutoka kwenye mkato wangu." Story ni ndefu. Nikarelate na mfanyakazi wangu wa zamani aliyewahi kutapeliwa kwa dawa hiyo hiyo na kulambwa 900,000 kwa kila chupa. yeye alinunua mbili tena kubwa kweli. Ndugu zangu kama siyo ujanja na kudra za Mwenyezi Mungu nilikuwa nitapeliwe jana. jihadharini sana hawa watu ni wajanja sana.UUUUWII!!!! BEWARE MY FRIENDS Breakdown ya faida ilikuwa iwe 600,000 x 50=30,000,000
toa 4,000,000 za Dr. Amos Mpacha toa 2,000,000 za Justin Masawe(former supp)
bal 24,000,000 tunagawana mimi na Cosmas Komba. Milioni 12,000,000 kirahisirahisi hivyo jamani? Acheni hizo!!

Anonymous said...

Ni jana tu (15th September) mwenyewe nimepigiwa simu na hawa jamaa with the very different status that wako TANAPA Moro but sikuwa na access na internet at that time so sikuweza kugoogle for the info about the vaccination(Gustarvick)with the deception scandal. Worse, the guy who presented himself to me with the product said that he got my 4n number from one of my friends so kwa haraka nikampigia huyo rafiki bt akakata cmu thn akanitumia txt akisema spika mbovu so nikamtext kumuuliza kuhusu uhalisia juu ya huyo jamaa 4rm TANAPA Moro nd she(rafiki yangu) verified dat anamjua kwa karibu sana ni shemeji yake so straightly nilimuamini bt wit doubts coz she used to be such a good texter bt texts zake zikawa na capital letters ki2 ambacho wengi ambao hawajui kutxt huwa inadhihilisha ni lack of writing skills na pia kutoa kisingizio cha spika mbovu ndo kabisa nikadoubt.... the same storry ikaendelea like previous victims bt this time imetokea dar na hotel ya Golden Tulip ikitumika na sio Double Tree and wakitumia tigopesa na sio mpesa km zamani.
Kwa upande wangu mimi sina pesa kabisa so hiyo laki 2.8 niliyopoteza ni somo kubwa sana (Nothing is for free) ambalo the money i was conned is nothing at all.... My point is these guys are so clever dat they can con u in a very different way, just usikubali to do anything with this medicine ...
Nitashughulika na huyu rafiki ambaye cmu yake imetumika... Again thnx for the info maana wanategemea wanitafute asubuhi yakuamkia leo(16th Sep)so nw i knw the answer to give them

Anonymous said...

Hahahaha mimi wamenipigia juzi tu hapa ila kwasababu nilishawahi wasikia ckushituka ila nilienda nao mpaka pale wanapotaka code namba ya mzigo sasa ilifika mahali mimi natakiwa kulipia 990,0000 hahaha waligandaje

Mtazamo News . Powered by Blogger.