WAFANYABIASHARA NCHINI TANZANIA WATAKIWA KUTUMIA BRELA KUSAJILI BIASHARA ZAO
Wafanyabiashara nchini Tanzania wametakiwa kutumia Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) kuweza kujisajili ili kuwawezesha kupata ulinzi shughuli zao hivyo pia kuwarahisishia kuweza kupata mikopo benki.
Wito huo umetolewa na Afisa Usajili Msaidizi Idara ya Makampuni majina ya
Biashara kutoka Wakala wa Usajili Biashara na Leseni (BRELA),Marry
Glory Mmari wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya biashara yaliyokuwa yakifanyika kwenye viwanja vya
Mwahako mjini Tanga.
Alisema wafanyabiashara wanapokuwa
wamesajiliwa kisheria na kupata majina ya biashara zao inawawezesha hata
wakati wanapokuwa wakiomba mikopo benki kupata kirahisi kutokana na
kwamba benki wanaweza kucheki nao na kuwaeleza huyo mtu amesajiliwa.
“Hivyo
nitoe wito kwa wafanyabiashara ambao hawajasajili watumie brela
kusajili biashara zao kwani inakuwa faida kwao kutokana na kwamba
anakuwa amepata ulinzi hivyo kumrahisishia kwenda benki kupata
mikopo”Alisema Marry Glory.
Ameeleza kuwa wameendelea kutoa
elimu kwa wafanyabiashara ,wananchi na wajasiriamali kuhusu shughuli
wanazozifanya na mwamko umekuwa mkubwa ambapo zaidi ya majina ya
Biashara 30 na makampuni 10 ikiwemo kuhuisha taarifa majina 10 ya
biashara kutoka kwenye mfumo wa zamani.
Alisema taarifa hizo
zilihuhishwa kutoka kwenye mfumo wa zamani kwenye kieletroniki huku
akieleza changamoto kubwa zilizokuwepo wakati wa kubailisha mfumo
alikuwa ni kazi kubwa kama mteja anakuwa amesahau taarifa zake.
Ili mteja aweze kusajili jina la kampuni anatakiwa kuwa
na akaunti, aina ya jina analosajili na namba ya nida ikiwemo simu na
barua pepe ili aweza kusajili jina la biashara.
Post a Comment