BENKI YA DUNIA YAAHIDI KUISAIDIA TANZANIA KUKABILIANA NA ATHARI ZA CORONA
Benki ya Dunia (WB) imefungua dirisha kwa Tanzania la
kusaidia kukabiliana na athari za janga la Uviko 19 katika Sekta mbalimbali
ikiwemo ya Utalii, biashara na bajeti ya Serikali.
Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba ametoa taarifa hiyo jijini Dodoma alipokutana na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji anayeziwakilisha Nchi za Kundi la Kwanza la Afrika katika Benki ya Dunia (AfG1 Constituency), Dkt. Taufila Nyamadzabo.
Dkt. Nchemba alisema
kuwa ugonjwa wa Uviko 19 umekuwa
na athari katika Bajeti ya Serikali kwa ujumla, kwa kuwa, kunapotokea
changamoto za kiuchumi katika nchi zinazofanya biashara na Tanzania huathiri makusanyo
ya kodi zinazotokana na uagizwaji na uingizaji
wa
bidhaa pamoja na mapato yatokanayo na ufanyaji wa biashara na nchi nyingine.
“Licha ya ahadi ya Benki
ya Dunia kuisaidia Tanzania katika kukabiliana na athari za Uviko 19, Benki
hiyo imeahidi kufungua miradi iliyokuwa imekwama kwa muda mrefu ukiwemo mradi wa
kuboresha miundombinu ya elimu ya Sekondari nchini, jambo ambalo ni la faraja
kwa Taifa kwa kuwa ni eneo ambalo tunalipa kipaumbele”, alieleza Dkt. Nchemba.
Mambo mengine yaliyojadiliwa ni pamoja na mwenendo wa Mfumuko wa Bei kwa Tanzania ambao
umeendelea kuwa kati ya asilimia 3 hadi 5, Deni la Taifa ambalo ni himilivu ambapo
deni la Serikali kwa uwiano wa Pato la Taifa ni asilimia 27.9 ili hali ukomo ni
asilimia 70 kwa kutumia vigezo vya Shirika la Fedha la Umoja wa Mataifa (IMF)
na Benki ya Dunia (WB), pamoja na mchango wa Benki ya Dunia katika kuweizesha
Sekta Binafsi nchini.
Mpaka sasa Bodi ya
Wakurugenzi ya Benki ya Dunia kwa kuidhinisha mikopo minne ya masharti nafuu
yenye jumla ya dola za Marekani bilioni 1.017 (sawa na shilingi trilioni
2.3391) kwa Serikali ya Tanzania kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya
maendeleo.
Miradi hiyo
ni ya kuboresha miundombinu ya barabara, kuimarisha mazingira ya ufundishaji na
mafunzo katika taasisi za elimu ya juu, kuongeza upatikanaji wa huduma bora za
mtandao na kuongeza wigo wa upatikanaji wa huduma bora za umeme visiwani
Zanzibar.
Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. Taufila Nyamadzabo, ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa
jitihada zake za maendeleo na kupunguza umasikini. Pia amesema kuwa Serikali
inatakiwa kuendelea kukusanya rasilimali kwa ajiri ya kukabiliana na athari za Uviko
19 na pia kutumia rasilimali hizo kikamilifu katika kutekeleza miradi ikiwemo
inayotolewa fedha na WB na kuishirikisha Sekta Binafsi katika miradi ya
maendeleo ili kuajiri vijana wengi zaidi.
Pia ameahidi kuwa
ataendelea kusimama kwa niaba ya Serikali ya Tanzania katika kuiwakilisha kwenye
Bodi ya Wakurugenzi wa WB ili kunufaika kwa ushirika wake na Benki ya Dunia,
hususan katika uidhinishaji wa fedha za miradi ya maendeleo.
Post a Comment