TANESCO YAWAPANDISHA KIZIMBANI WATU SABA
Baadhi ya watuhumiwa hao wakisindikizwa na polisi kwenye mahakama ya hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Disemba 2, 2020.
Shirika
la Umeme Tanzania ( TANESCO) limewapandisha kizimbani watu sita katika Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam Desemba 2, 2020 kwa
tuhuma za kuingilia miundombinu ya umeme na kulisababishi Shirika
hasara ya shilingi milioni sita.
Watuhumiwa hao ni pamoja na Boniphace Emmanuel, Elitruda Ancelim, Twalib Ibrahim, Mwarami Omary, Vumilia Sultani Kaambi, James Joseph na Haidary Islamy.
Hata hivyo upande wa mashtaka umesema upelelezi bado unaendelea na haukuwa na kipingamizi katika kutolewa dhamana ambapo hakimu anayesikiliza kesi hiyo alisema kila mshtakiwa anapaswa kulipa shilingi milioni moja na kuwa na mdhamini mmoja ambaye sharti awe mtumishi wa Umma.
Kesi imehairishwa hadi tarehe Disemba 16 mwaka huu.
Post a Comment