MTANGAZAJI

UPENDO ZAIDI WAHITAJIKA KWA WANAOISHI NA VVU

 


Mkurugenzi wa REPPSI Edwick Mapalala akiwa katika maonyesho ya siku ya ukimwi katika viwanja vya Posta, Kijitonyama

 

Mkurugenzi Mkazi wa Shirika  Regional Psychosocial Support Initiative (REPPSI), Edwick Mapalala ameikumbusha jamii kuongeza upendo na kuendelea kutokomeza unyanyapaa kwa watu wanaoishi na Virusi vya Ukimwi (VVU).

Amesema kuwalinda, kuwathamini na kuwajali watu wanaoishi na VVU hasa vijana kutasaidia kuwapunguzia msongo wa mawazo wale ambao hawajaikubali afya yao, na hivyo kuikubali na kushiriki katika kukuza uchumi wa Taifa.
Mapalala amesema hayo wakati akitoa salamu za REPPSI, Shirika linalojihusisha na malelezi, makuzi na msaada wa Kisaikolojia kwa watoto kuhusu siku ya Ukimwi Duniani.

“Hii ni siku ya kutafakari kuhusu maambukizi ya VVU, waliopima na kujua afya zao waendelee kuwa waaminifu kwenye utumiaji wa dawa, wasiopima wapime ili wajitambue na wale wasio na maambukizi"amesema Mapalala.

Akizungumzia mradi wa Ready Plus, unaowahusu vijana wanaoishi na VVU Mapalala amesema wengi wamejikubali, wanajiamini na wanaendeleza ndoto zao za kimaisha baada ya kupatiwa elimu sahihi kuhusu VVU
.
“Na nitoe wito kwa jamii, tuendelee kuwalea vijana wetu kwa upendo, tusiwakatishe tamaa kwa sababu wanaweza kufikia ndoto,” amesema Mapalala.

Hata hivyo ameipongeza Serikali ya Tanzania kwa jitihada kubwa katika kupambana na VVU.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.