MTANGAZAJI

TBS YATEKETEZA VIPODOZI VYENYE VIAMBATA SUMU

Zoezi la uteketezaji wa vipodozi vyenye viambata sumu vya thamani zaidi ya shilingi
milioni 125 likiendelea mwishoni mwa wiki, Zoezi hilo limeteketezwa na TBS Jijini Arusha.

  Shirika la Viwango Tanzania (TBS) limeteketeza vipodozi vyenye viambata sumu vya thamani ya Shilingi milioni 125 baada ya kufanyika kwa ukaguzi wa kushitukiza
kwenye maghala ya kuhifadhia vipodozi ambayo hayajasajiliwa.


Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa mwishoni mwa wiki na TBS,Vipodozi hivyo vilivyopigwa marufuku vilikutwa katika maghala la kampuni ya Kimario Cosmetics hivi karibuni na wakaguzi wa TBS Jijinii Arusha na kukamatwa kwa mujibu wa Sheria ya Viwango Na. 2 ya mwaka 2009 pamoja na  Marekebisho yake ya Mwaka 2019.


“Mmiliki wa ghala hilo Pamphil L. Kimario amelipa shilingi milioni 3.5 ikiwa ni
gharama ya kuteketeza bidhaa hizo hatarishi kwa afya ya binadamu kwani
zinapotumiwa huweza kusababisha madhara mbambali kwa mtumiaji”,Inasisitiza
taarifa hiyo Taarifa hiyo imeeleza kuwa, Baadhi wa Watanzania wamekuwa  wakitumia vipodozi hivyo vyenye viambata vya sumu ambavyo vina kemikali ya Mercury na Hydoroquinone kwa lengo la kung’arisha ngozi zao na hata kubadili rangi ya ngozi hizo bila kujali madhara yatokanayo na bidhaa hizo.

 
Vipodozi vyenye kemikali ya Mercury kwa Mujibu ripoti ya Shirika la Afya
Duniani(WHO) ya mwaka 2020, vikitumika kwa muda mrefu vinasababisha magonjwa ya figo, mapafu, ngozi, macho mfumo wa fahamu mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na mfumo wa kinga ya mwili na kwa upande wa matumizi ya vipodozi vyenye kemikali ya hydroquinone husababisha magonjwa ya kansa ya ngozi.


Aidha, Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Sheria ya Fedha Na. 8 ya mwaka 2019 iliipa
Mamlaka TBS ya kusimamia usajili wa bidhaa za chakula ,vipodozi , maghala ya
kuhifadhia chakula na vipodozi pamoja na migahawa na mahoteli jukumu lillilokuwa likifanywa hapo awali na iliyokuwa Mamlaka ya Dawa Chakula na Vipodozi (TFDA).


Utekelezaji wa Sheria hiyo ya Fedha ulianza rasmi tangu Julai 2019, hivyo kuwalazimu wauzaji wazalishaji na wauzaji wa vipodozi kusajili bidhaa hizo pamoja na maghala ya kuhifadhia.


Shirika pia limeteketeza bidhaa nyingine zisizofaa za vipodozi na vyakula
zilizokamatwa katika kaguzi zilizofanyika nyakati tofauti katika maeneo mengine
Arusha na nje ya Arusha katika kipindi cha Januari hadi Novemba 2020.


TBS inaendelea na ukaguzi huu nchi nzima pamoja na kuwahimiza wazalishaji na
wauzaji wa vipodozi kuhakikisha kuwa wanafuata taratibu zilizopo kwa kusajili bidhaa hizo pamoja na maghala ili kuepuka usumbufu. Pia wauzaji wa vipodozi wanahimizwa kuwa na orodha ya bidhaa za vipodozi visivyoruhusiwa ambayo inapatikana katika tovuti ya Shirika www.tbs.go.tz

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.