UONGOZI SAO HILL WATOA MIEZI MIWILI KWA WAKANDARASI KUKAMILISHA UJENZI WA MABWENI
Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Sao Hill Juma Mwita akipa maelezo wakati wa kukagua miradi ya ujenzi wa mabweni |
TFS kupitia Shamba la Miti Sao Hill linatekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika jamii inayozunguka shamba ikiwa ni pamoja na ujenzi wa mabweni katika shule za sekondari.
Wakati
wa ukaguzi wa miradi hiyo Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Miti Sao Hill Juma
Mwita amesema lengo za ukaguzi wa miradi ni kuhakikisha miradi hii
inakamilika kwa wakati kama ilivyokusudiwa.
Hata
hivyo Mwita aliwataka wajenzi na wasimamizi wa miradi ya ujenzi wa
mabweni kuhakikisha miradi hii inakamilika ndani ya miezi miwili ili
wanafunzi wanapofungua shule mwezi Januari mabweni hayo yaweze kutumika.
"Lengo
la mabweni haya ni kusaidia watoto wetu wa kike ili wakae mahali salama
wakiwa shuleni na hii itasaidia sana wanafunzi hao kusoma katika
mazingira mazuri."Alisema Mhifadhi Mkuu wa Shamba
Mwita
aliongeza kuwa TFS inasaidia jamii katika miradi mbalimbali ikiwa ni
sehemu ya kuonyesha shukrani na kuwakumbusha wananchi kuendelea kulinda
misitu iliyopo kwa faida mbalimbali zinazoonekana.
Naye
Mwalimu Paul Msukwa kutoka Shule Sekondari Ihanu alisema kuwa mabweni
haya yatawasaidia sana wanafunzi wa kike kuondokana na changamoto
zinazowakabili na itasaidia ufaulu kupanda.
"Mabweni
haya mawili yaliyokaguliwa ambayo yapo katika Shule ya Sekondari
Luganga na Ihanu yatakuwa na uwezo wa kuchuka wanafunzi 160 kwa wakati
mmoja" alisema
Post a Comment